EACC yakamilisha awamu ya kwanza ya uchunguzi dhidi ya KEMSA

Tume ya maadili na kupambana na ufisadi-EACC imekamilisha uchunguzi kwenye awamu ya kwanza ya sakata ya halmashauri ya usambazaji dawa nchini-KEMSA ambapo nchi hii ilipoteza mabilioni ya pesa.

Mwenyekiti wa tume ya EACC, Askofu mkuu mstaafu Eliud Wabukala, alisema wamewachunguza maafisa wote wa umma waliohusika kwenye sakata hiyo na kukabidhi faili hizo kwa mkurugenzi wa mashtaka ya umma.

Also Read
Zoezi la kukusanya saini milioni 4 kwa ajili ya BBI kuzinduliwa Jumatano

Akiwahutubia wanahabari katika hoteli ya Naivasha wakati wa warsha ya mafunzo ya siku mbili kwa maafisa wa ununuzi bidhaa na wale wa masuala ya kifedha kutoka halmashauri ya ujenzi wa barabara kuu, Wabukala alisema tume ya EACC sasa inaanza uchunguzi kuhusu zaidi ya kampuni 80 ambazo zimekuwa zikinufaika na fedha kutoka kwa halmashauri hiyo ya serikali.

Also Read
Kaunti tano zachunguzwa kwa ufujaji wa fedha za kukabiliana na Covid-19

Wabukala  ambaye hakutangaza mapendekezo waliotoa alisema kwamba mfumo wa ununuzi bidhaa katika halmashauri ya KEMSA unahitaji kurekebishwa kwani una kasoro nyingi.

Aidha alisema tume hiyo mwaka huu imetwaa mali za thamani ya shilingi bilioni 6.2 na zaidi ya shilingi milioni 208 pesa taslimu zilizotokana na ufisadi.

Also Read
Lusaka adinda kufanyia marekebisho mswada wa marekebisho ya katiba wa mwaka 2020

Kadhalika aliongeza kusema kwamba katika muda wa miaka mitano iliyopita tume ya EACC imekamilisha kushughulikia kesi 824 zinazohusiana na ufisadi ambapo hukumu zimetolewa kwa kesi 153.

  

Latest posts

Justin Muturi kuwania urais kwa tiketi ya chama cha DP

Tom Mathinji

Bunge lapendekeza kuchunguzwa kwa mfumo wa ununuzi wa KEMSA

Tom Mathinji

Serikali yatoa chakula cha msaada kwa wanaokabiliwa na njaa nchini

Tom Mathinji

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi