EACC yasema imetwaa mali ya mabilioni ya pesa iliyopatikana kupitia ufisadi

Tume ya maadili na kupambana na ufisadi-EACC imesema kuwa imepiga hatua muhimu katika vita dhidi ya ufisadi katika kipindi cha miaka mitatu iliopita.

Akihutubia baadhi ya wafanyakazi wa halmashauri ya bandari nchini katika kituo cha kuhifadhia mizigo cha Nairobi,kamishna wa tume hiyo Dkt.Dabar Malim alisema tume hiyo imeshawasilisha kesi mahakamani na wahusika kuwajibishwa.

Also Read
Wakili wa Sonko kwenye kesi ya ufisadi ajiondoa

Kulingana na Dabar tume hiyo imeimarisha mbinu za uchunguzi wa ufisadi na kurejesha mali zilizopatikana kwa njia za ufisadi ili kukomesha kashfa hizo.

Also Read
Maangi, Osoro wakamatwa muda mchache kabla kuhudhuria mazishi ya Nyachae

Dabar alisema kwamba mafanikio ya tume hiyo yanajumuisha kurejeshwa kwa mali ya thamani ya takriban shilingi bilioni 26.5, shilingi bilioni 135.9 zilizokuwa zimeporwa na wafisadi na watu 293 kufunguliwa mashtaka.

Kamishna huyo aliwahimiza wafanyakazi wa halmashauri hiyo kuzingatia madili ili iweze kuimarika zaidi.

Also Read
Nalaumu wapinzani wangu kwa tuhuma za ufisadi - Ojaamong asema

Aidha aliwapongeza wakuu wa halmashauri hiyo kwa kuandaa warsha hiyo ya kuhimiza maadili katika uongozi na kuwasaidia kuweka mikakati ya kuwawezesha kupamba na ufisadi na kuwa mfano bora wa utoaji wa huduma kwa umma.

  

Latest posts

Shule za umma zina uwezo wa kuandikisha matokeo bora iwapo zitajikakamua zaidi

Tom Mathinji

Musalia Mudavadi apuuzilia mbali dhana ya ma-‘Hustler’

Tom Mathinji

Wafungwa watoroka katika gereza la Nanyuki usiku wa manane

Tom Mathinji

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi