EACC yawachunguza Magavana wanne kwa kujipatia mali kwa njia tatanishi

Tume ya maadili na kukabiliana na ufisadi imesema kuwa kwa sasa inawachunguza magavana wanne kuhusiana na sakata ya kujipatia mali ya thamani ya shilingi bilioni-11 kinyume cha sheria.

Tume hiyo pia inafuatilia mali ya thamani ya takriban shilingi bilioni-25 zilizoachwa na maafisa wa umma zilizopatikana kwa njia zisizoeleweka.

Akiongea alipofika mbele ya kamati ya Senate kuhusu haki, maswala ya kisheria na haki za binadamu, mwenyekiti wa tume ya EACC askofu mkuu mstaafu Eliud Wabukula, alisema tume hiyo imekamilisha uchunguzi wa kesi sita za ngazi za juu zinazowahusisha magavana tisa walioko na wale wa zamani wa kaunti za Tharaka-nithi, Nairobi, Kiambu, Garissa, Samburu, Busia, Migori na Nyandarua.

Also Read
Waliotekeleza ghasia za baada ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2007/2008 mashakani
Also Read
EACC yafanya msako wa ghafla katika afisi za KEMSA

Wabukala pia alisema kuwa tume hiyo imekamilisha uchunguzi kuhusiana na madai ya kujipatia mali kinyume cha sheria na kwa njia zisizoeleweka dhidi ya magavana wa zamani Ferdinand Waititu, Mike Sonko, Evans Kidero na Moses Kassaine.

Alisema kesi hizo zingali zinaendelea mahakamani na pia kasoro katika ununuzi wa bidhaa na huduma za umma katika shirika la KEMSA, kusubiri tathmini ya mkurugenzi wa mashtaka ya umma.

Also Read
EACC yasema imetwaa mali ya mabilioni ya pesa iliyopatikana kupitia ufisadi

Wakati huo huo Wabukala aliibua wasiwasi kuhusiana na changamoto ya ukosefu wa pesa za kutosha katika tume hiyo, kuingizwa kwa siasa katika vita dhidi ya ufisadi na mienendo isiyofaa na pia mfumo hafifu wa kisheria wa kutekeleza sura ya sita ya katiba.

  

Latest posts

Shule za umma zina uwezo wa kuandikisha matokeo bora iwapo zitajikakamua zaidi

Tom Mathinji

Musalia Mudavadi apuuzilia mbali dhana ya ma-‘Hustler’

Tom Mathinji

Wafungwa watoroka katika gereza la Nanyuki usiku wa manane

Tom Mathinji

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi