Ebrahim Raisi anusia kiti cha Urais katika uchaguzi mkuu nchini Iran

Mgombeaji wa kiti cha Urais nchini Iran mwenye msimamo mkali, Ebrahim Raisi ambaye alikuwa mkuu wa idara ya mahakama, anaongoza kwenye kinyanganyiro cha uchaguzi wa urais, baada ya asilimia-90 ya kura kuhesabiwa.

Awali, wagombeaji wengine watatu kati ya wanne kwenye kinyanganyiro hicho, walitangaza kukubali kushindwa saa chache tu kabla ya wizara ya masuala ya ndani kutangaza matokeo ya uchaguzi huo.

Also Read
Wito watolewa wa kurejeshwa kwa polisi wa akiba Laikipia

Raisi ambaye ni mwandani wa kiongozi wa kidindi nchini Iran, Ali Hosseini Khamenei, alipigiwa upatu wa kuibuka mshindi kwenye uchaguzi huo, uliokumbwa na idadi ndogo ya wapiga kura na kuchujwa kwa wagombeaji wengi.

Wagombeaji wawili kwenye uchaguzi huo, Abdolnaser Hemmati na Amir Hossein Ghazizadeh Hashemi wamempongeza Raisi kwa ushindi wake.

Hata hivyo Raisi hajazungumzia tangazo la Hermmati na aliyekuwa kamanda wa kikosi maalum cha Revolutionary Guard,Mohsen Rezaei la kushindwa kwenye kinyanganyiro hicho.

Also Read
Israeli yaonya kuhusu ufaafu wa Rais Mteule wa Iran Ebrahim Raisi

Raisi mwenye umri wa miaka 60, amehudumu wadhifa wa kiongozi wa mashtaka kwa muda mrefu. Aliteuliwa jaji mkuu mwaka 2019, miaka miwili baada ya kushindwa na Hassan Rouhani katika uchaguzi mkuu uliopita.

Raisi amenyooshewa kidole cha lawama na raia wengi pamoja na makundi ya kutetea haki za binadamu nchini Iran, kwa mauaji ya wafungwa wengi wa kisiasa katika miaka ya themanini. Kulingana na shirika la Amnesty International, Raisi alikuwa mmoja wa majaji wanne waliowahukumu kifo wafungwa 5,000.

Also Read
Wahudumu wa boda boda watakiwa kuzingatia sheria za barabarani kikamilifu

Hata hivyo kiongozi huyo wa kidini ameahidi kubuni nafasi za ajira pamoja na kuondoa vikwazo ambavyo nchi hiyo iliwekewa na Marekani vinavyosababisha mateso mengi ya kiuchumi hasaa kwa wananchi wa kawaida.

  

Latest posts

Mwanafunzi ateketeza bweni kukwepa kufanya mitihani Tharaka Nithi

Tom Mathinji

Mahakama yamzuia Mohammed Badi kuhudhuria mikutano ya Baraza la Mawaziri

Tom Mathinji

IEBC yalenga kuwasajili wapiga kura wapya milioni sita kabla Uchaguzi Mkuu ujao

Tom Mathinji

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi