Embarambamba aahidiwa usaidizi na Ezekiel Mutua

Mwanamuziki kutoka eneo la Kisii ambaye amekuwa akizungumziwa sana kwenye mitandao ya kijamii kutokana na namna anacheza kwenye video za muziki wake Embarambamba ana kila sababu ya kutabasamu kutokana na ahadi ya Daktari Ezekiel Mutua.

Mkurugenzi huyo mkuu wa bodi ya kuorodhesha filamu nchini KFCB alitoa ahadi hiyo baada ya kutizama mahojiano ya msanii huyo kwenye kituo kimoja cha runinga humu nchini.

Daktari Mutua alisema kwenye mitandao ya kijamii kwamba msanii huyo kwa jina halisi Christopher Mosioma alisema kwamba sarakasi zake za kubiringika chini kwenye matope na kuparamia vitu ni kutokana na umasikini na anatafuta usaidizi.

Also Read
KFCB: Wanaohusika na utovu wa maadili miongoni mwa vijana kunaswa

Hapo ndipo Mutua, aliamua kumwalika na kuahidi kutafuta njia ya kumsaidia akisema sarakasi zake ni za aibu ilhali yeye mwenyewe anasikika kama aliye na akili timamu.

Embarambamba mzaliwa wa eneo la Kisii ni mwanamuziki ambaye alianza kwa kuimba nyimbo za kidunia na baadaye kugeukia nyimbo za injili lakini mtindo wake wa kucheza anapopatiwa nafasi ya kutumbuiza ni ule ule.

Also Read
Gucci Mane asajili mwanamuziki mwingine

Yeye hukumbia mbali na jukwaa na hata kuangukia umati wakati mwingine, pale anapoparamia hema. Video za nyimbo zake ambazo yeye husambaza kupitia mitandao ya kijamii zimeundwa katika eneo moja kijijini ambapo anakimbiakimbia kwenye mashamba, kupanda mit na kujiangusha kutoka juu na wakati mmjoa alipanda ng’ombe ambaye alimbwaga chini.

Also Read
Baba Ijesha aachiliwa kwa dhamana

Awali Dr. Mutua alisema anahisi kwamba mwanamuziki huyo anahatarisha maisha yake na mashabiki wanamshangilia akijiumbua. alishangaa kama mtindo wake ni endelevu huku akitaka akatazwe na kuzuiwa asitekeleze visanga vyake.

Kwenye mahojiano kadhaa mwanamuziki huyo amesikika akiomba usaidizi ili kupata vifaa vya kutayarisha video za nyimbo zake kwani kwa sasa anatumia rununu.

  

Latest posts

Betty Bayo Afichua Sura ya Mpenzi Wake

Marion Bosire

Mr. Seed Asimulia Safari Yake ya Muziki

Marion Bosire

Rick Ross Azungumzia Uhusiano Wake na Hamisa Mobeto

Marion Bosire

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi