Engin Firat kuiga Harambee Stars Jumatatu baada ya mechi ya Rwanda

Kocha mkuu wa Harambee Stars Engin Firat ataigura timu hiyo Jumatatu baada ya mchuano wa mwisho wa kundi E kufuzu kwa fainali za kombe la dunia dhidi ya Rwanda Novemba 15 katika uwanja wa kitaifa wa Nyayo.

Also Read
Mabondia watano wa Kenya waepuka mchujo wa kwanza mashindano ya Dunia AIBA

Firat alisaini mkataba wa miezi miwili na FKF ambapo alipaswa kuisimamia Kenya , katika mechi 4 zilizokuwa zimesalia za kufuzu kombe la dunia ambazo zitakamilika Jumatatu.

Mktaba wake ulikuwa uongezwe endapo angeifuzisha Kenya kwa raundi ya tatu ya kombe la dunia lakini tayari hayo yote yametubuka ,Stars ikiwa ya 3 kwa alama 3 pekee.

Also Read
Meneja wa Gor Mahia FC Jolawi Obondo awekwa pembeni kwa siku 30

Raia huyo wa Uturuki awali alikuwa kocha wa Moldova alipoangoza kwa mechi 11 kushindwa 9 na kutoka sare mbili.

Also Read
Tusker Fc kuondoka nchini Jumanne kwenda Alexandria kuikabili Zamalek Ijumaa

Kamati ya muda inayoongozwa na jaji mstaafu Aaron , ilitwaa usimamizi wa soka nchini Kenya Ijumaa huku FKF ikivunjiliwa mbali na waziri wa michezo Dkt Amina Mohammed kutokana na uongozi mbaya na ufujaji wa pesa.

  

Latest posts

Amos Kipruto ashinda London Marathon huku Jepkosgei akimaliza wa pili kwa vipusa

Dismas Otuke

Malkia Strikers wabanduliwa mashindano ya dunia baada ya kipigo cha seti 3-1 na Puerto Rico

Dismas Otuke

Boubacar Kamara kutocheza kwa muda kutokana na Jeraha

Tom Mathinji

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi