‘Engineer’ Olunga arejea kwa vishindo kuwanusuru Al Duhail SC katika ligi ya mabingwa barani Asia

Nahodha wa Harambee Stars Michael Olunga alirejea kuichezea klabu yake ya Al Duhail SC kwa kishindo ,alipopachika bao la pekee na ushindi katika mchuano wa kundi D,wa ligi ya mabingwa barani Asia (AFC) dhidi Sepahan ya Iran mjini Buraidah, nchini Arabia Jumapili usiku.

Also Read
Olunga azidi kuwatesa makipa Japan

Olunga ambaye ni mfungaji bora katika ligi kuu nchini Qatar ,alikuwa amekosa mechi ya ufunguzi ya kundi hilo,tarehe 7 April ,wakati timu yake ilipocharazwa mabao 2-1 nyumbani dhidi ya Al Taawoun, .

Also Read
Shujaa wako tayari kwa Olimpiki asema nahodha Ambaka

Mshambulizi huyo wa Kenya aliye na umri wa miaka 28 aliibuka mfungaji bora msimu jana wa ligi ya mabingwa barani Asia kwa magoli 9.

Also Read
Kenya iko tayari kwa Kipkeino Classic asema mkurugenzi wa mashindano Barnaba Korir

Matokeo ya Jumapili usiku yanaweka wazi kundi D ,kila timu ikiwa na alama 3,Pakhtakor,Al Tawoon,Sepahan na Al Duhail SC.

  

Latest posts

Amos Kipruto ashinda London Marathon huku Jepkosgei akimaliza wa pili kwa vipusa

Dismas Otuke

Malkia Strikers wabanduliwa mashindano ya dunia baada ya kipigo cha seti 3-1 na Puerto Rico

Dismas Otuke

Boubacar Kamara kutocheza kwa muda kutokana na Jeraha

Tom Mathinji

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi