Eric Omondi aachiliwa kwa dhamana

Mchekeshaji huyo alikamatwa jana alasiri na maafisa wa upelelezi wa jinai na wale wa bodi ya kuorodhesha filamu nchini KFCB kwa kosa la kuunda na kusambaza kipindi bila idhini.

Ameachiliwa hii leo kwa dhamana ya shilingi elfu hamsini na atafikishwa mahakamani Alhamisi tarehe 18 mwezi huu wa Machi mwaka 2021.

Mkurugenzi mkuu wa KFCB Ezekiel Mutua ndiye alitangaza kukamatwa kwa mchekeshaji huyo kutokana na kipindi ambacho anatayarisha na kusambaza kwenye mitandao cha “Wife Material”.

Also Read
Emmanuel Ehumadu ashutumiwa kwa kukusanya pesa za mazishi ya Asuzu

Kabla ya hapo Chipukeezy ambaye pia ni mchekeshaji na rafiki wa karibu wa Eric Omondi alionekana kumuunga mkono huku akimhakikishia kwamba kuna mazuri siku za usoni.

Alipachika picha ya Eric akiwa ameshika tuzo mbili na kuandika usemi wa Victor Pinchuk ambaye ni mfanyibiashara wa Ukraine kwamba sanaa, Uhuru na ubunifu vitabadili ulimwengu haraka kuliko siasa.

Wakili Karen Nyamu pia amemtetea Eric kupitia akaunti zake za mitandao ya kijamii akisema kwamba amekuwa akisaidia vijana wengi kupata riziki wakati huu ambapo hakuna nafasi za kazi kwa vijana.

Kulingana naye, kuna njia bora ambazo wanaokerwa na awamu ya pili ya kipindi cha Wife Material wangetumia kando na kukamata na kushtaki wasanii.

Wakili huyo anaonelea kwamba kuwakamata na kuwashtaki wasanii sio njia bora ya kusimamia na kuorodhesha kazi za sanaa nchini Kenya.

  

Latest posts

Waigizaji Wa Nollywood Wazuru Zanzibar kwa Fungate

Marion Bosire

Betty Kyallo Apata Kazi ya Kuigiza

Marion Bosire

Gurdian Angel Asifia Mpenzi Wake

Marion Bosire

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi