Eric Omondi aahirisha ‘Wife Material 2’

Mchekeshaji Eric Omondi wa humu nchini ametangaza kwamba kipindi chake cha mitandaoni cha Wife Material 2 kitaanza tarehe 17 mwezi Mei mwaka huu wa 2021.

Kipindi hicho kilikuwa kianze tena wiki hii lakini kimesadifiana na mfungo wa mwezi mtukufu wa Ramadhan ambao unaanza kesho Jumatano tarehe 14 mwezi Machi.

Omondi ambaye hijiita rais wa wachekeshaji barani Afrika alielezea kwamba watano kati ya waigizaji wa kipindi hicho ni waumini wa dini ya kiisilamu.

Also Read
Filamu nyingine ya Kenya kuonyeshwa kwenye Netflix

Zaidi ya hapo, mchekeshaji huyo aliendelea kwa kutetea kazi yake ya sanaa akisema sekta ya burudani imetoka mbali tangu enzi za kina Mzee Ojwang ambaye alikuwa muigizaji mchekeshaji na Daudi Kabaka mwanamuziki.

Kilingana naye mtu anayekosa kukua anakufa kitalanta na anasema sekta ya burudani nchini Kenya lazima ikue na ijipatie nafasi kwenye ulimwengu wa digitali uliojaa ushindani tele.

Also Read
Embarambamba aahidiwa usaidizi na Ezekiel Mutua

“Ulimwengu umepunguzwa kuwa kijiji kidogo kupitia mtandao na ninalazimika kushindana na majukwaa kama Netflix, YouTube, HBO, na Hollywood yenyewe.” aliandika Eric.

Anasema wakati alianza kutumbuiza kwenye kipindi cha Churchill Live mwaka 2008 mambo yalikuwa tofauti na angeafikia lengo la kuchekesha umati kwa vichekesho vinavyohusu lugha za kabila mbali mbali nchini lakini sasa mambo ni tofauti.

Kulingana naye, wasiposonga jinsi ulimwengu unasonga wataangamia kitaaluma. Aliahidi kuendelea kuwepo hata baada ya miaka 13 ya uchekeshaji ambapo atakua, ajibadili na ajivumbue upya kwa miaka mingi.

Also Read
Mwambieni Diamond ninampenda

Jukumu lake anasema linajumuisha kuburudisha wakenya akitafuta kushindana na wengine barani Afrika na kuibuka mshindi mwishowe.

Na ikiwa lengo ni kushinda barani na ulimwenguni, alisema mipango lazima ibadilike.

  

Latest posts

Wasanii Wanaowakilisha Kenya AFRIMA

Marion Bosire

Akothee Apata Mgeni wa Heshima Kwenye Hafla Yake

Marion Bosire

KFCB Yazuia Usambazaji Wa Filamu

Marion Bosire

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi