Eric Omondi amekamatwa

Mkurugenzi mkuu wa bodi ya kuorodhesha filamu nchini Kenya KFCB Dakta Ezekiel Mutua ndiye alitangaza haya kupitia ukurasa wake wa Facebook jioni ya leo.

Kulingana naye, maafisa kutoka KFCB na wale wa idara ya upelelezi wa jinai walimkamata mchekeshaji Eric Omondi kwa kile ambacho anakitaja kuwa kukiuka sheria za kutayarisha filamu na hata michezo ya kuigiza jukwaani kwa kuunda na kusambaza kipindi kwa jina “Wife Material.”

Also Read
Mazishi ya Othuol Othuol

Taarifa ya Bw. Mutua inasema kwamba Eric Omondi atafikishwa mahakamani kwa kuvunja sheria.

Sheria ya filamu na michezo ya kuigiza nambari 222 inaelekeza ifuatavyo, kati ya mambo mengine mengi;

(1) Hakuna atakayeonyesha au kusambaza filamu ikiwa hajasaliwa kama muonyesha filamu au msambaza filamu na bodi husika na kupatiwa cheti.

Also Read
Eric Omondi apanua wigo anapotafuta mke!

(2) Hakuna filamu itakayosambazwa au kuonyeshwa hadharani au faraghani kabla ya kukaguliwa na bodi ya filamu ambayo itaiidhinisha kwa kutoa cheti.

(3) Yeyote atakayeonyesha filamu bila kuzingatia nambari ya kwanza na ya pili hapo juu, atakuwa ametenda kosa.

Mutua aliendelea kusema kwamba Bodi ya kuorodhesha filamu itachukua hatua zote za kisheria ili kusimamisha utayarishaji na usambazaji wa filamu zote ambazo hazijaidhinishwa kwenye jukwaa lolote la watu wengi.

Also Read
Eric Omondi apimana nguvu na Diamond Platnumz

Jambo lingine ambalo alikumbusha umma ni kwamba ni jukumu lao kama bodi kulinda watoto dhidi ya kazi za sanaa ambazo huenda zikawadhuru na kwa hivyo kila mmoja anayehusika na uundaji wa filamu lazima afuate sheria ya filamu na michezo ya kuigiza kifungu nambari 222.

  

Latest posts

Waigizaji Wa Nollywood Wazuru Zanzibar kwa Fungate

Marion Bosire

Betty Kyallo Apata Kazi ya Kuigiza

Marion Bosire

Gurdian Angel Asifia Mpenzi Wake

Marion Bosire

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi