Ethiopia yakaribisha wito wa kurejelewa mazungumzo na majirani wake kuhusu bwawa katika mto Nile

Wizara ya mashauri ya nchi za kigeni ya Ethiopia, imefurahia wito wa baraza la usalama la umoja wa mataifa wa kurejelea mazungumzo na nchi jirani za Misri na Sudan, ili kutanzua mzozo ulioko na kukamilisha makubaliano kuhusu mpango wa kujaza maji kwenye bwawa la (Gerd), yaani “The Grand Ethiopian Renaissance Dam”.

Also Read
MP Shah yazindua mtambo wa kutengeneza hewa ya Oxygen

Aidha, wizara hiyo ilifurahia hatua ya baraza la usalama, ya kuelekeza swala hilo kwa muungano wa nchi za Afrika (AU).

Kwa upande wake, wizara ya mashauri ya nchi za kigeni ya Misri imehimiza wapatanishi wote kufanikisha juhudi za kuafikia makubaliano.

Mradi huo wa bwawa la maji kwenye mto Blue Nile, umesababisha malumbano kati ya Ethiopia na majirani zake, huku Misri na Sudan zikiibua wasi wasi kwamba kutakuwa na ukame na uhaba wa maji.

Also Read
Utawala wa Taliban watakiwa kubuni serikali inayowajumuisha wote

Misri inachukulia mradi huo kuwa tishio kubwa kwa raia wake ikizingatiwa kwamba nchi hiyo inategemea mto huo wa huduma zote za maji, Ilhali Ethiopia inachukulia bwawa hilo kuwa njia ya pekee ya kuzalisha umeme na kusambazia ma-milioni ya raia wake.

Also Read
Kutakuwa na maziwa ya bure siku ya kusherehekea kupandishwa hadhi kwa mji wa Nakuru

Awali Umoja wa Mataifa ulihimiza mataifa hayo matatu kuafikia makubaliano ya kudumu kuhusu njia za kujaza maji kwenye bwawa hilo la kuzalisha umeme

  

Latest posts

Idara ya Mahakama yashutumiwa kwa kuhujumu shughuli muhimu za serikali

Tom Mathinji

Uhuru Kenyatta: Usalama wa taifa hili ni shwari

Tom Mathinji

Hospitali ya Kijeshi yazinduliwa katika kambi ya kijeshi ya Kahawa

Tom Mathinji

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi