Evelyn Wanjiru apeleka huduma Tanzania

Mwimbaji wa nyimbo za injili hapa nchini Kenya Bi. Evelyn Wanjiru amekuwa nchini Tanzania wikendi hii ambayo imekamilika kwa mwaliko wa kwaya iitwayo Essence of Worship.

Kwaya hiyo ilimwalika mwimbaji huyo kwa usiku wa sifa Ijumaa tarehe 18 mwezi huu wa Juni mwaka 2021, ambao pia ulikuwa wa kurekodi video za nyimbo kwa njia ya moja kwa moja.

Also Read
John Cena afunga ndoa

Tukio hilo lililopatiwa jina la “The night of my worship” lilifanyika katika kanisa la City Christian Church, saa mbili usiku hadi asubuhi.

Akiwa Tanzania Evelyn ambaye alikuwa ameandamana na mume wake aliyepia mtayarishaji wa muziki Agundabweni Akweyu mmiliki wa Bwenieve productions, alihojiwa kwenye vituo mbali mbali vya redio Kama vile Wasafi Fm.

Also Read
Wasafi Tv yafungwa kwa miezi sita

Alichapisha video ambayo inamwonyesha akichezea wimbo wake uitwao “Mungu Mkuu” pamoja na mtangazaji wa kipindi cha Wasafi Sunday Worship Lilian Mwasha.

Alipotoka Wasafi Fm, Wanjiru alihudhuria ibada ya Jumapili katika kanisa la Victory Christian Centre katika eneo la Mbezi Beach jijini Dar Es Salaam.

Also Read
Christine Mosha apatiwa kazi na Sony Music Africa

Kundi jingine ambalo Evelyn Wanjiru alikutana nalo Dar Es Salaam ni Zabron Singers maarufu kwa wimbo wao “Tumeuona mkono wake bwana”.

Waimbaji hao walimshangaza kwa kuimba tafsiri ya lugha ya kikuyu ya wimbo huo wao kwa ufasaha mkubwa.

  

Latest posts

Adasa Afichua Sababu ya Kimya Chake

Marion Bosire

Harmonize Matatani Tena

Marion Bosire

Pday Hurrikane Azungumzia Uhusiano Wake na Nyota Ndogo

Marion Bosire

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi