Fahamu timu 8 zitakazopiga robo fainali ya ligi ya mabingwa Afrika

Vilabu vinane vitakavyocheza kwota fainali ya ligi ya mabingwa Afrika ,imebainika kufuatia kumalizika kwa mechi za makundi Jumamosi iliyopita.

Timu nane zilizotinga robo fainali ni ;Simba sports Club ya Tanzania,Al Ahly ya Misri za kutoka kundi A,Mamelodi Sundowns ya Afrika Kusini na  CR Belouizdad ya Algeria za kundi B,Wyadad Casablanca kutoka Moroko na Kaizer Chiefs ya Afrika Kusini,Esperance ya Tunia na Mc Alger ya Algeria za kundi D.

Algeria na Afrika Kusini  inawakilishwa na timu 2 kila moja,wakati Tanzania,Tunisia,Moroko na Misri zikiwa na timu moja kila moja.

MC Alger-ilibuniwa mwaka 1962 ikiwa timu ya kwanza ya dini ya Kiislamu nchini Algeria

Inafunzwa na kocha Abdelkadir Amrani na itakuwa ikishiriki hatua ya robo fainali kwa mara ya nne  na ya kwanza tangu mwaka 1980 na kwa jumla watakuwa wakicheza kwota fainali kwa mara ya 8 ,miaka ya 1976 walipoibuka mabingwa,1977,1979,1980,2000,2011 na 2018.

Also Read
Mabingwa wa dunia Shelly-Ann Fraser-Pryce na Tajay Gayle kuiwakilisha Jamaica Olimpiki

CR Belouizdad  au Chabab Riadhi de Belouizdad  ni timu ya Algeria iliyobuniwa mwaka 1962  na itakuwa ikishiriki kombe la ligi ya mabingwa kwa mara ya  4 na ya kwanza tangu mwaka  2001 ingawa ni mara ya kwanza kucheza robo fainali.

Belouizdad wameshiriki kombe hilo miaka ya 1970,2001 na 2002 huku wakibanduliwa katika raundi ya kwanza kwenye makala yote.

Wydad Athletic  Club  au maarufu Wydad Casablanca ni timu ya Moroko  iliyobuniwa mwaka 1937 na inaongozwa na kocha Faouzi Benzarti.

WAC inashiriki ligi ya mabingwa kwa mara ya 12 mwaka msimu huu na wametawazwa mbaingwa mwaka wa 1992 na 2017 na pia walicheza hadi robo fainali msimu wa mwaka 2019-2020.

Al Ahly ni timu ya Misri iliyobuniwa mwaka 1907 na ni miongoni mwa timu kongwe zaidi Afrika.

Also Read
Timu za Kenya za Cestoball kutangazwa wakati wa majaribio ya kitaifa kati ya tarehe 13 na 17 mwezi ujao

Ahly maarufu kama Red Devils ndio timu iliyoshinda kombe la ligi ya mabingwa Afrika mara nyingi zaidi ikiwa mara 9 na inaongozwa na kocha Pitso Mosimane.

Ahly wanatetea kombe hilo msimu huu .

Mamelodi Sundowns ukipenda Masandawana au the Brazzillians ni klabu ya Afrika Kusini iliyobuniwa mwaka 1970 na wanashiriki ligi ya mabingwa Afrika kwa mara ya 14 wakitawazwa mabingwa mwaka 2016 na watakuwa wakicheza kwota fainali kwa mara ya 6.

Kaizer Chiefs ukipenda  Amakhosi  na ilibuniwa mwaka 1970  na inafunzwa na kocha Gavin Hunt.

Chiefs wamefuzu kwa robo fainali ya ligi ya mabingwa Afrika kwa mara ya kwanza .

Esperance sportive du Tunis  ni klabu ya Tunisia  inashiriki kombe la ligi ya mabingwa msimu huu kwa mara ya 19  na kuibuka mabingwa mara 4 mwaka 1994,2011,2018  na 2019  .

Also Read
CECAFA ya vlabu vya akina dada kuingia nusu fainali Jumatatu

Simba sports club ndio mwakilishi pekee wa Afrika mashariki na ukanda wa Cecafa aliyefuzu kwa robo fainali ya mwaka huu ikiwa pia mara ya kwanza katika historia ya ligi ya mabingwa Afrika.

Timu nane zilizofuzu kwa hatua ya robo fainali zimegawanywa katika makundi mawili ,viongozi wa makundi na timu zilizonyakua nafasi za pili.

Katika kwota fainali timu zilizoongoza makundi zimetanganishwa na zitapangwa dhidi ya wapinzani waliomaliza nafasi ya pili lakini timu zilikuwa kundi moja hazipangwa pamoja .

Hata hivyo hali itabadilika wakati wa droo ya semi fainali ambapo timu yoyote itapangwa na mpinzani yeyote.

Mabingwa wa kombe hilo watafuzu kuhsiriki kombe la dunia baina ya vilabu.

 

 

 

 

  

Latest posts

Police Fc washerehekea kurejea ligi kuu baada ya mwongo mmoja kwa dhifa

Dismas Otuke

Sportpesa kurejesha ufadhili michezo nchini Kenya

Dismas Otuke

Vidosho wa Kenya wapigwa dafrao na Msumbiji mashindano ya kikapu Afrika

Dismas Otuke

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi