Faith Kipyegon asajili muda wa nne wa kasi duniani katika mita 1500

Bingwa wa Olimpiki Faith Kipyegon alisajili muda wa kasi wa nne duniani katika mbio za mita 1500 katika mkondo wa 6 wa mashindano ya Diamond League mjini Monaco Ufaransa Ijumaa usiku.

Kipyegon ambaye pia ni mshindi wa medali ya fedha ya dunia aliziparaka mbio hizo kwa dakika 3 sekudne 51 nukta 7, ambayo ni rekodi ya kitaifa huku akimshinda bingwa wa dunia Sifan Hassan wa Uholanzi aliyeibuka wa pili kwa dakika 3 sekunde 53 nukta 60 .

Also Read
Gor Mahia walenga hatua ya makundi ligi ya mabingwa CAF kwa mara ya kwanza

Shindano hilo lilikuwa la mwisho kwa wanariadha hao wawili huku wakijiandaa kumenyana tena kuwania dhahabu ya Olimpiki mapema mwezi ujao mijini Tokyo Japan.

Faith Kipyegon baada ya kuandikisha rekodi mpya ya kitaifa

Bingwa wa dunia mwaka 2015 katika mita 3000 kuruka viunzi na maji Hyvin Kiyeng aliandikisha muda wake bora msimu huu akishinda kwa dakika 9 sekunde 3 nukta 82 akifuatwa na bingwa mtetezi wa dinia Beatrice Chepkoech kwa dakika 9 sekunde 4 nukta 94 huku Winfred Mutile wa Bahrain akichukua nafasi ya tatu.

Also Read
Mabingwa wa Olimpiki na dunia Kipyegon na Chepkoech kushiriki mkondo wa 6 wa Moanco Diamond league
Hyvin Kiyeng akiruka kiunzi katika mita 3000 

Bingwa wa dunia Timothy Cheruiyot aliweka muda wa kasi akiibuka mshindi wa mita 1500 kwa dakika 3 sekunde 28 nukta 28 ambao pia ni muda bora wa kibinafsi akifuatwa na Mohamed Katir wa Uhispania kwa dakika 3 sekunde 28 nukta 76 naye bingwa wa ulaya Jakob Ingebrigtsen akaridhia nafasi ya tatu kwa dakika 3 sekunde 29 nukta 25.

Also Read
Kasait ,Obiri na Faith Kipyegon wajikatia tiketi za Olimpiki
Timothy Cheruiyot baada ya kushinda mita 1500

Abraham Kibiwot alichukua nafasi ya pili katika mita 3000 kuruka viunzi na maji kwa dakika 8 sekunde 7 nukta 81 ,nyuma ya Lamecha Girma wa Ethiopia aliyetimka kwa dakika 8 sekunde 7 nukta 75 .

Emmanuel Korir pia aliibuka wa pili katika mita 800 akitumia dakika 1 sekunde 43 nukta 04 nyuma ya Nijel Amos wa Botswana aliyeibuka mshindi kwa dakika 1 sekunde 42 nukta 91.

  

Latest posts

Police Fc washerehekea kurejea ligi kuu baada ya mwongo mmoja kwa dhifa

Dismas Otuke

Mwanafunzi ateketeza bweni kukwepa kufanya mitihani Tharaka Nithi

Tom Mathinji

Mahakama yamzuia Mohammed Badi kuhudhuria mikutano ya Baraza la Mawaziri

Tom Mathinji

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi