Familia ya afisa wa IEBC aliyetoweka yazungumza

Familia ya msimamizi wa uchaguzi katika eneo bunge la Embakasi mashariki Daniel Mbolu Musyoka imetoa wito kwa taasisi za usalama kuharakisha juhudi za kumtafuta jamaa wao ambaye alitoweka alhamisi iliyopita.

Also Read
Mahakama ya upeo yaamrisha IEBC kufungua sava na masandaku ya kura ya vituo 15

Mbolu alitoweka muda mfupi kabla ya kutangaza matokeo ya uchaguzi wa eneo-bunge la Embakasi mashariki.

Siku tatu baada ya kisa hicho, mkewe Tabitha Mbolu, anasema familia yake inahangaika kwa sababu juhudi zote za kumtafuta mpendwa wao hata kwenye makafani na hospitalini hazijafaulu.

Also Read
Wakenya waonywa dhidi ya kutoa jumbe za kupotosha

Bi. Mbolu aliyeongea nyumbani kwao Nyonjoro katika eneo-bunge la Bahati, kaunti ya Nakuru alisema mara ya mwisho kuwasiliana na mumewe ilikuwa jumatano tarehe 10 mwezi Augosti.

Also Read
Sofapaka,Talanta FC na Police FC wasajili ushindi ligi kuu

Familia yake imesema polisi waliripoti kwamba simu yake ya mkononi ilizimwa saa moja baada ya kutoweka kwake katika sehemu ya mihango, utawala.

  

Latest posts

Wakazi wa Baragoi wahimizwa kuishi kwa amani

Tom Mathinji

Malkia Strikers warejea nyumbani kinyemela baada ya kubanduliwa mashindano ya dunia

Dismas Otuke

CAF yafungua maombi ya maandalizi ya fainali za AFCON mwaka 2025

Dismas Otuke

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi