Familia ya DMX yafafanua mambo kadhaa

Siku moja tu baada ya kifo cha mwanamuziki wa Marekani DMX mambo mengi yalichipuza kwenye mitandao ya kijamii kama vile umiliki wa rekodi asilia za muziki wake yaani master tapes na mchango wa hela za kufadhili mazishi yake.

Ilisemekana kwamba wanandoa Beyonce Knowles na Jay Z ambao pia ni wanamuziki walikuwa wamenunua rekodi asilia za muziki wa DMX na wakazitoa kama zawadi kwa watoto wake.

Also Read
Anderson .Paak atoa onyo

Taarifa nyingine zilidai kwamba kuna watu ambao wameanzisha michango kwa kutumia jina la marehemu wakiisingizia kuwa ya kufadhili mazishi yake.

Kutokana na hayo, familia ya marehemu Earl Simmons au ukipenda Dark Man X imefafanua kupitia taarifa rasmi kwamba hakuna yeyote ambaye amenunua rekodi asilia za DMX na kwamba hawachangishi pesa zozote kwa ajili ya mazishi ya mpendwa wao.

Also Read
Trey Songz akamatwa

Familia hiyo ilisema pia kwamba hakuna bidhaa ambazo wanaunda na kuuza kwa jina la marehemu DMX ili kuchangisha pesa. Walitoa tahadhari kwamba yeyote ambaye anachangisha pesa za mazishi ya DMX ni tapeli.

Jamii ya DMX kupitia kwa taarifa hiyo hiyo iliahidi kujuza umma kuhusu mipango ya mazishi ya mwanamuziki huyo tajika.

Also Read
Familia ya DMX yatoa taarifa kuhusu hali yake hospitalini

DMX aliaga dunia Ijumaa tarehe 9 mwezi Aprili mwaka huu wa 2021 baada ya kulazwa katika chumba cha wagonjwa mahututi cha hospitali ya White Plains kwa wiki moja.

Anasemekana kupata mshtuko wa moyo baada ya kutumia kiasi kikubwa cha madawa ya kulevya kwa wakati mmoja.

  

Latest posts

Rayvanny Kumtambulisha Msanii wa Kwanza NLM

Marion Bosire

Dulla Makabila Ajiondolea Lawama

Marion Bosire

Mwigizaji Atoa Ilani Kwa Rais Museveni

Marion Bosire

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi