Familia ya marehemu Ayimba yahitaji shilingi milioni 2 nukta 7

Familia ya aliyekuwa kocha wa timu ya taifa ya raga ya Kenya kwa wachezaji 7 kila upande  Benjamin Ayimba imewaomba wakenya kujitokeza kuchangia gahrama ya matibabu iliyoachwa na marehemu pamoja na gharama ya mazishi.

Akizungumza na wanahabari Jumatatu jioni mjombake marehemu Ayimba,Joseph Ayimba alisema wameruhisiwa kuchukua mwili wa marehemu kutoka Hospitali kufuatia agizo la serikali lakini wanadaiwa shilingi milioni 1 nukta 7 ikiwa gharama ya matibabu pamoja na ya kuhifadhi mwili na nyingine milioni 1 kutayarisha mazishi.

Also Read
Shujaa yamaliza ya pili mkondo wa kwanza wa Solidarity Camp mjini Stellenbosch

“Tunawaomba Wakenya kuendelea kutoa mchango wao kupitia kwa  paybill 8021673 jina la akaunti ni Benjamin Otieno Ayimba Medical ,kwa sasa tuna upungufu wa shilingi milioni 2 nukta 7,milioni 1 nukta 7 ikiwa bill ya hospitali  iliyoachwa na marehemu huku milioni moja ikiw agharama ya  mazishi “akasema Joseph Ayimba

Also Read
Shujaa yashindwa fainali ya kombe kuu na Afrika Kusini 5-38 Vancouver 7's

Msemaji wa familia hiyo Oscar Osir amesema kuwa mipango ya mazishi tayari imeanza huku marehemu akitarajiwa kuzikwa baada ya siku 14.

“Tunatarajia kuandaa mazishi baada ya wiki mbili kutoka leo,tutakua na ibada ya marehemu katika kanisa la Holy Family Basilica Siku ya Jumatano,na kuwa na kesho ya maombi hapa rfuea Ijumaa kabla ya kusafiri kwenda kwa mazishi yatakayoandaliwa Jumamosi eneo la Uranga kaunti ya Siaya”akasema Osir

Also Read
Ni rasmi michezo ya Olimpiki kuandaliwa bila mashabiki wa kigeni

Chama cha raga pia kimeanza mikakati ya kuandaa mashindano kama kumbukumbu kwa marehemu kwa mjibu wa mwenyekiti wa KRU Oduor Gangla.

“tunajadiliana na wadau mbalimbali kuhusu kuandaa mashindano ya kumkumbuka na kumuenzi marehemu”akasema Gangla

  

Latest posts

Sportpesa kurejesha ufadhili michezo nchini Kenya

Dismas Otuke

Vidosho wa Kenya wapigwa dafrao na Msumbiji mashindano ya kikapu Afrika

Dismas Otuke

FKF yakatiza mkataba wa shilingi milioni 127 na Odibets

Dismas Otuke

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi