FC Talanta yavishwa taji ya NSL huku Vihiga Bullets ikipandishwa hadi ligi kuu FKF kwa mara ya kwanza

FC Talanta ambayo ni timu inayomilikiwa na mamlaka ya mawasiliano nchini Kenya ,ndio mabingwa wa mwaka huu wa ligi kuu ya soka ya daraja ya pili almaarufu National Super League (NSL) , baada ya kupokea kombe lao Jumapili jioni katika uwanja wa GEM Cambridge international school.

Also Read
Kenya yaiduwaza Zambia mechi ya kirafiki Nyayo

FC Talanta wamepandishwa ngazi kushiriki ligi kuu ya Kenya msimu ujao baada ya kuibuka mabingwa wa NSL kwa alama 72 kutokana na michuano 37 , wakishinda 21,kutoka sare 9 na kushindwa 7 huku wakifunga mabao 52 na kufungwa 29.

Also Read
Mashemeji wasusia Derby ya Jumamosi hadi FKF itoe posho ya Milioni 3

Vihiga Bullets walichukua nafasi ya pili kwa alama 64 kufuatia kusajili ushindi wa ambao 2-0 dhidi ya Kibera Black Stars uwanjani Bukhungu siku ya Jumapili na pia kupandishwa ngazi kucheza ligi kuu msimu ujao kwa mara ya kwanza.

Also Read
City Stars waizidia maarifa Bandari Fc ligi kuu FKF

Kenya Police walimaliza katika nafasi ya tatu baada ya kusajili ushindi wa magoli 2-1 ugenini dhidi ya Migori Youth na watacheza mchujo dhidi ya Vihiga United ambapo mshindi atafuzu kucheza ligi kuu msimu ujao.

  

Latest posts

Kenya Simbas yanusurika na kufuzu kwa fainali ya kombe la Afrika

DOtuke

Injera na Onyala kukosa nusu fainali ya Algeria baada ya kujeruhiwa

DOtuke

KBC yafadhili timu ya magari itakayoshiriki mashindano ya Machakos Rallycross

DOtuke

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi