Filamu kupelekwa mashinani

Daktari Ezekiel Mutua mkurugenzi mkuu wa bodi ya kuorodhesha filamu nchini KFCB amefichua kwamba hivi karibuni watafufua tena ule mpango wa zamani wa kupelekea wananchi filamu katika sehemu mbali mbali.

Akizungumza katika mahojiano kwenye kipindi cha runinga ya KBC cha Good Morning Kenya, Daktari Mutua alisema kwamba jukumu kubwa la bodi yake ni kudhubiti kazi ya sanaa ili kuhakikisha inatimiza mahitaji ya kimaadili lakini wanapoona mianya wanaishughulikia kama bodi.

Also Read
Ringtone amwonya Eric Omondi

Jinsi KBC kwa ushirikiano na wizara ya Teknolojia ya mawasiliano na maswala ya vijana ilianzisha Studio Mashinani ili kutoa nafasi kwa wanamuziki kurekodi nyimbo zao, Mutua anasema watashirikiana na KBC na wadau wengine ili kupeleka filamu mashinani.

Alitetea kazi ambayo KFCB inafanya ya kuhakikisha maadili yanazingatiwa katika kazi za sanaa akisema wakati umefika wa kupiga gumzo kuhusu maadili.

Also Read
Juma Nature ateuliwa balozi wa Temeke

Kulingana naye, wazazi wa sikuhizi hawana muda wa kukaa na watoto ili kuwakuza kimaadili kwa hivyo mengi wanajifunza kupitia runinga na hivyo Kuna haja ya kuhakikisha kazi safi ndiyo inaonyeshwa.

Wanatumia mbinu ya kuchagua mabalozi wa kuhimiza kazi safi kimaadili ambapo alitaja Walter Mong’are maarufu kama nyambane ambaye ni balozi wa kitaifa.

Mahojiano ya Ezekiel Mutua yamejiri siku chache baada yake na Eric Omondi kuvutana mitandaoni kutokana na usemi wake kwamba wasanii hawana pesa.

Also Read
Siku ya Kimataifa ya Busu

Kwa sababu hiyo Eric Omondi alichapisha video inayoonyesha akiwa ametandaza noti za pesa ambazo alisema zilikuwa jumla ya shilingi milioni tatu akisema sanaa inalipa.

Usemi wa Ezekiel ulitokana na kitendo cha Eric Omondi cha kumpa msanii Kevin Bahati pesa baada ya KFCB kudinda kufadhili kama ilivyokuwa imeahidi.

  

Latest posts

Zuchu Amtania Mamake Khadija Kopa

Marion Bosire

Muigizaji Jaymo Afunga Ndoa

Marion Bosire

Don Jazzy Anatafuta Kumsajili Salle

Marion Bosire

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi