Filamu za Kenya katika jukwaa la kimataifa

Kesho Ijumaa tarehe 9 mwezi Oktoba mwaka huu wa 2020, filamu nyingine ya Kenya itazinduliwa kwenye jukwaa la kimataifa la filamu kwa jina “Netflix”.

Kazi hiyo ya ubunifu ambayo mwelekezi wake ni Nick Mutuma inajulikana kama “Sincerely Daisy” na ni ya pili kuingia Netflix kutoka Kenya baada ya kazi nyingine kwa jina “Poacher” kuwekwa huko mwisho wa mwezi Septemba mwaka huu.

Also Read
Serikali Yatia Saini Mkataba na Netflix

Nick Mutuma alitangaza hayo kupitia akaunti yake ya Instagram siku chache zilizopita. Sincerely Daisy ni hadithi ya msichana ambaye amekamilisha elimu ya shule ya upili ambaye ana tamaa ya kufanya vizuri maishani na mahusiano yake ya kimapenzi.

Filamu ya tatu kutoka nchini Kenya ambayo itaingia katika jukwaa la Netflix ni “Disconnect” ambayo ni toleo la mwaka 2018.

Also Read
Eddy Kenzo Atilia Shaka Uhusiano Wake na Bobi Wine

Kazi hiyo ni ya vichekesho na waliogiziza ni Brenda Wairimu, Nick Mutuma, Patricia Kihoro, Pascal Tokodi, Catherene Kamau, Pierra Makena na Brian Ogola.

Sekta ya filamu nchini Kenya ipo na wadau hujikaza kutengeneza kazi ambazo zinakubalika ila kuna vikwazo kadhaa ambavyo vimesababisha kazi hizo zisifikie upeo wa kimataifa.

Watayarishaji filamu nchini Kenya hulalamikia mahitaji mengi kutoka kwa serikali ndipo wapate vibali vya kuunda filamu na pia kuna ugumu wa kufikia maeneo ya kutengeneza filamu ambayo mengi hulipiwa.

Also Read
Butita Anasherehekea Siku Yake ya Kuzaliwa

Kuna pia tatizo la ukosefu wa ushirikiano kati ya watayarishaji filamu. Tatizo jingine ni hatua ya serikali kupiga marufuku kazi za ubunifu labda kwa kile ambacho kinaonekana kama ni ukiukaji wa maadili.

  

Latest posts

Filamu ya Kenya yashinda tuzo nchini Nigeria

Tom Mathinji

Just A Band yarejea tena baada ya kimya cha muda

Tom Mathinji

Yul Edochie Azungumzia Ndoa Yake ya Wake Wawili

Marion Bosire

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi