FKF yakosolewa kwa kumtimua kocha Jacob Mulee wakati usiofaa

Shirikisho la soka nchini Kenya FKF limekosolewa kwa kumtimua kocha wa timu ya taifa Harambee Stars Jacob Mulee na wasaidizi wake  Twahir Muhidin na Hagai Azande.

Kulingangana na Tom Alila aliyekuwa mwanachama wa kamati kuu ya NEC katika FKF miaka ya nyuma , haukuwa wakati mwafaka kumtimua kocha Mulee na wadaidizi wake Twahir Muhidin na Hagai Azande , wakati Kenya inapojiandaa kwa mechi mbili za mwezi ujao kufuzu kombe la dunia dhidi ya Mali.

Also Read
Gor Mahia tayari kuwashika mateka wanajeshi APR Jumamosi

“Kwanza tunataka kujua ni kwa nini kocha Mulee na wasaidizi wake walipigwa kalamu,lakini FKF ingewaruhusu makocha hao kusimamia mechi za mwezi ujao jabla ya kuwatimua, huku ni kurudisha timu nyuma “akasema Alila

Also Read
Uwanja wa Bin Ali utakaondaa kipute cha kombe la dunia mwaka 2022 wazinduliwa

Hata hivyo Alila ambaye pia alikuwa mwaniaji wa NEC Nairobi katika uchaguzi uliopita ,amesisitiza kwamba ili Kenya kufanya vyema inapaswa kumrejesha Francis Kimanzi au kumteua kocha wa kigeni .

“Sasa tunataka wamrejeshe Francis Kimanzi kwa sababu anaelewa timu hiyo la sivyo watafute kocha wa kigeni ambaye atakuwa huru kuchagua wachezaji bila mapendeleo wala kushurutishwa.

Also Read
Safari ya kwenda AFCON 2021 yarejea

Pia ilikuwa makosa kwa Victor Wanyama na wachezaji wengine kuachwa nje ya Harambee stars bado anahitajika kuleta tajriba” akaongeza Alila.

Harambee stars itachuana na Mali mjini Yaounde tarehe 6 mwezi ujao katika kundi E kufuzu kwa kombe la dunia kabla ya kuwaalika Mali siku chache baade.

Kenya imezoa alama 2 kutokana ba mechi mbili za kundi E .

  

Latest posts

Mabondia watano wa Kenya waepuka mchujo wa kwanza mashindano ya Dunia AIBA

Dismas Otuke

Timu 16 zitakazoshiriki hatua ya makundi ya ligi ya mabingwa Afrika zabainika

Dismas Otuke

Kipchoge atawazwa mwanariadha bora wa Olimpiki kwa wanaume

Dismas Otuke

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi