Shirikisho la soka FKF limelalamikia kuhusu ukosefu wa viwanja nchini kuandaa mechi za ligi kuu na mashindano ya kimataifa.
Kulingana na katibu mkuu wa FKF Bari Otieno wanalazimika kuandaa mechi za ligi kuu katika viwanja duni baada ya serikali kuwazuia kutumia viwanja vya Nyayo na Kasarani.
“imekuwa vigumu kuandaa mechi za ligi kuu na pia hata za kimataifa kwa sababu hatuna viwanja kwa sasa ,tunachezea katika viwanja vibovu na vya hali duni,tunaiomba serikali ituruhusu kutumia viwanja vya Nyayo na Kasarani ambavyo viko katika hadhi inayohitajika”akasema Otieno
Kenya inapaswa kuandaa mashindano ya kombe la cecafa kwa wanawake kuanzia tarehe 17 mwezi huu hadi Agosti mosi mwaka huu.
Fainali ya kombe la FKF Betway siku ya Jumipili kati ya AFC Leopards na Gor Mahia ilipaswa kaundaliwa katika uwanja wa Utalii kabla ya kuhamishiwa Nyayo.
Mechi za ligi kuu Kenya zimekuwa zikindaliwa kaunti ya Nairobi katika uwanja mdogo ulie nje ya uga wa Kasarani,ule wa Utalii na Ruaraka na michuano mingine katika uwanja wa manispaa ya Thika.