FKF yatangaza kurejea kwa ligi kuu Mei 12 na kukamilika Agosti 28

Shirikisho  la kandanda nchini FKF limetangaza kuanza kwa mechi za raundi ya pili kuwania ligi kuu Fkf tarehe 12 mwezi huu.

Kwa mjibu wa ratiba hiyo  Afc Leopards itawaalika Mathare United Jumatano ijayo katika uwanja wa Kasarani kabla ya Gor Mahia kumenyana na Wazito Fc baadae jioni katika uwanja wa Kasarani .

Also Read
Harambee Stars yarejea nyumbani kujiandaa kukabiliana na Rwanda Jumatatu

Mechi moja ya raundi ya 17 itachezwa Mei 14 , huku mapambano mengine 7 ya mzunguko huo yakipigwa kati ya Mei 16 na 17.

Msimu wa sasa wa ligi kuu unatarajiwa kukamilika tarehe  28 mwezi Agosti mwaka huu.

Also Read
FKF yasukuma mbele kuanza kwa ligi kuu kutoka Mei 12 hadi Mei 14

Tusker Fc ingali kuongoza msimamo kwa alama 36 baada ya michuano 16 ikifuatwa na Kenya Commercial Bank kwa alama 30 huku  Afc Leopards ikishikilia nafasi ya 3 kwa pointi 30.

Ligi hiyo ilisitishwa mwezi mmoja uliopita na Rais Uhuru Kenyatta katika tangazo la kusimamisha michezo yote nchini kama njia ya kuzuia msamabo wa Covid 19.

Also Read
Zaidi ya wanariadha 400 kushiriki mashindano ya Agnes Tirop Cross Country Classic Jumamosi hii

Hata Hivyo Wizara ya michezo inasubiriwa kutoa uamuzi baada ya kushauriana na wizara ya afya kuhusu tarehe mpya ya kurejelwa kwa shughuli za michezo nchini.

  

Latest posts

Malkia Strikers wabanduliwa mashindano ya dunia baada ya kipigo cha seti 3-1 na Puerto Rico

Dismas Otuke

Boubacar Kamara kutocheza kwa muda kutokana na Jeraha

Tom Mathinji

Kenya kukabana koo na Puerto Rico mechi ya mwisho ya kundi A mashindano ya dunia

Dismas Otuke

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi