Gabon itachuana na Burkina Faso katika mchuano wa kwanza wa raundi ya 16 bora kuwania kombe la Afcon nchini Cameroon.
Gabon maarufu kama Panthers watapambana na The Stallion ya Burkina Faso kwenye mechi ya tarehe 23 mwezi huu.

Gabon ilimaliza ya pili kutoka kundi C wakati ,Burkina Faso pia ikichukua nafasi ya pili kutoka kundi B.
Timu nyinginezo zilizofuzu kwa awamu ya 16 bora ni pamoja na wenyeji Cameroon,Senegal,Guinea,Morocco,Gabon na Nigeria,huku nafasi zilizosalia nane zikijazwa baina ya Jumatano na Alhamisi.

Michuano ya raundi ya 16 bora itachezwa kati ya tarehe 23 na 25 mwezi huu,kabla ya kupisha kwota fainali Januari 29 na 30 ,nazo semi fainali zipigwe Februari 2 na 3 na hatimaye fainali Februari 6.