Gatlin na Omanyala tayari kuonyesha ubora wao Kip Keino Classic Jumamosi

Bingwa mara tatu wa dunia Justin Gatlin kutoka Marekani amesema yuko tayari kudhihirisha ubora wake atakapotimka mbio za mita 100 katika mkondo wa 12 na wa mwisho wa mashindano ya Kip Keino  Classic Jumamosi jioni.

Gatlin aliye na umri wa miaka 39 kwenye mahojiano na wanahabari Ijumaa amesema kuwa anataka kusajili matokeo bora kwenye shindano hilo litakalokuwa la mwisho kwake mwaka huu ili kuwatumbuiza na kuwafurahisha mashabiki wake.

Also Read
Cheptegei na Gidey wavunja rekodi za dunia
Justin Gatlin

“Sikujua nina wafuasi wengi hivi huku Kenya,likiwa shindano langu la mwisho mwaka huu nataka kufunga msimu vizuri na kuwaburudisha “akasema Gatlin

“Ni mara yangu ya kwanza kuja Kenya na pia itakuwa mara yangu ya kwanza kushindana Kenya niko tayari Jumamosi” akaongeza Gatlin

Also Read
Safaricom Lewa Marathon kuandaliwa kupitia mtandao Juni 26
Omanyala na Gatlin

Ferdinand Omanayala wa Kenya aliyeandikisha historia aliposhiriki Olimpiki kwa mara ya kwanza na kufikia nusu fainali atakabaliana na Galtin kwenye mbio za Jumamosi uwanjani Kasarani.

“Niko tayari na nataka kudhihirisha kuwa ninao uwezo ,na kushindana na mtu kama Gatlin ni fahari sana”akasema Omanyala

Also Read
Hansi Flick asaini kandarasi ya miaka mitatu kuinoa Ujerumani

Shindano la mita 100 wanaume litawashirikisha Gatlin,Omanyala,Japka Jeremiah kutoka Nigeria Mouhamadou Fall na Amoury Gotlin wote wa Ufaransa pamoja na Wamarekani Mike Rodgers,King Tyree na Travon Bromell wa Marekani ambaye ndiye mwanariadha mwenye kasi zaidi mwaka huu katika mita 100.

Mbio hizo zitaanza saa kumi na mbili kasoro dakika 10 jioni.

  

Latest posts

Tusker waleweshwa nyumbani na Zamalek 1-0

Dismas Otuke

Tysa yasherekea miaka 20 ya kubadilisha vijana Kitale kupitia soka

Dismas Otuke

Ni Siku ya Ndovu kumla mwanawe Tusker dhidi ya Zamalek Nyayo

Dismas Otuke

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi