Gavana mteule wa Meru Kawira Mwangaza ajiunga na Kenya Kwanza

Gavana mteule wa kaunti ya Meru Kawira Mwangaza, amejiunga na muungano wa Kenya Kwanza, siku chache baada ya kushinda wadhifa wa Ugavana na kumpiga kumbo Kiraitu Murungi.

Mwakilishi huyo mwanamke wa zamani wa kaunti ya Meru aliyewania wadhifa wa Ugavana akiwa muwaniaji huru, alipata kura  209,148, dhidi ya mshindani wake wa karibu wa Mithika Linturi wa chama cha UDA aliyepata kura  183,859 huku Kiraitu Murungi akiwa wa tatu kwa kupata kura110,814.

Also Read
Matayarisho ya uchaguzi mkuu yakamilika Samburu
Also Read
Mbunge wa Tiaty William Kamket aachiliwa huru

Kawira alipata uungwaji mkono kutoka kaunti nzima ya Meru, huku akipata kura nyingi katika maeneo bunge sita kati ya tisa katika kaunti hiyo. Katika eneo bunge la Imenti kusini nyumbani kwa Kiraitu Murungi, Kawira alipata kura 31,921 dhidi ya Kiraitu aliyepata kura  22,359.

Also Read
Tifa: Naibu Rais William Ruto ndiye muwaniaji Urais maarufu zaidi

Katika uchaguzi mkuu wa mwaka  2013, alijiunga na siasa na kuwania kiti cha ubunge cha Buuri ambapo alikuwa wa pili.

  

Latest posts

Maendeleo ya Wanawake yampongeza Rais kwa kuwateuwa wanawake mawaziri

Dismas Otuke

NMS yakabidhi majukumu yake kwa kaunti ya Nairobi

Tom Mathinji

Hamisi Massa ateuliwa kaimu Mkurugenzi wa idara ya DCI

Tom Mathinji

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi