Gavana Muriithi atoa wito wa mjadala wa kuboresha ripoti ya BBI

Gavana wa Kaunti ya Laikipia Ndiritu Muriithi ametoa wito wa mjadala wa kuboresha ripoti ya mpango wa maridhiano wa kitaifa, BBI.

Muriithi amesema viongozi wanafaa kufahamu kuwa utayarishaji wa katiba ni mchakato wa muda mrefu, kwa hivyo ipo haja ya mjadala wa manufaa kuhusu ripoti hiyo ili kuiboresha.

Also Read
Mudavadi ajitosa rasmi ulingoni huku mwangwi wa BBI ukivuma kote nchini

“Tujadiliane tulete mawazo ambayo yanaweza kuendesha Kenya mbele. Isiwe kila saa ni matusi ambayo hayana maana,” amesema Muriithi.

Muriithi, aliyekuwa akiongea mjini Nyahururu amesema ripoti hiyo ina mapendekezo yanayostahili lakini inafaa kuboreshwa ili kuimarisha ugatuzi kwa kupandisha hadhi ya Bunge la Seneti miongoni mwa masuala mengine.

Also Read
Musalia Mudavadi: Rais Kenyatta hanipigii debe kuwa mridhi wake

Amesema magavana ni sharti wahakikishe kuwa mapendekezo yanayohusiana na nyongeza ya pesa kwa maeneo ya kaunti yamekitwa kwenye ripoti hiyo.

Also Read
Raila aelezea matumaini kuwa Mabunge 24 ya kaunti yataidhinisha mswada wa BBI

Gavana huyo amesema suala la kuchelewa kutoa pesa kwa maeneo ya kaunti sharti lishughulikiwe na BBI.

Baraza la Magavana limependekeza marekenbisho makubwa yapatayo matano kwenye ripoti hiyo ya BBI.

 

  

Latest posts

Serikali yatoa chakula cha msaada kwa wanaokabiliwa na njaa nchini

Tom Mathinji

Daktari aliyewaua wanawe wawili kaunti ya Nakuru amefariki

Tom Mathinji

Shule 43,000 kote nchini kuunganishiwa mtandao wa internet

Tom Mathinji

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi