Gavana Mutua apinga uamuzi wa Mahakama kuhusu Magavana wanaotaka Urais

Kiongozi wa chama cha Maendeleo Chap Chap Dkt. Alfred Mutua amepinga uamuzi wa mahakama kwamba magavana walio na azma za kuwania urais wanafaa kujiuzulu wadhifa huo miezi sita kabla ya uchaguzi.

Mutua ambaye ni Gavana wa Kaunti ya Machakos amesema kuwa uamuzi huo wa mahakama sio wa haki na unawabagua magavana.

Also Read
Chuo kikuu cha Taita Taveta kuanza mafunzo ya uhandisi wa mafuta na Petroli

Gavana Mutua ambaye tayari ametangaza nia ya kuwania urais kwenye uchaguzi mkuu wa mwaka wa 2022 amesema kuwa uamuzi huo ni sharti upingwe ili kuhakikisha usawa.

Also Read
Wamiliki wa vyumba vya wageni Machakos washtumiwa kwa kuvigeuza mabaa

“Kenya inapaswa kuwa nchi inayohimiza usawa ili watu wote wanaotaka kugombania kiti cha juu zaidi nchini wapewe nafasi sawa ya kushindana,” akasema.

Mutua amesema haya kwenye hafla ya kutia sahihi mkataba wa makubaliano kuhusu uimarishaji wa kilimo cha majini katika Kaunti ya Nyeri.

Also Read
NCIC yataka mamlaka zaidi kukabiliana na matamshi ya chuki

Vile vile ametoa wito kwa viongozi kuheshimiana huku nchi hii ikikaribia uchaguzi mkuu.

Ametoa wito wa usawa katika utekelezaji wa sheria kuhusu kupiga marufuku mikusanyiko ya hadhara lakini pia akawahimiza viongozi kuheshimu sheria.

  

Latest posts

Wanjigi: Kenya haina uwezo kuwapa wasio na ajira shilingi 6,000 kila mwezi

Tom Mathinji

Mwanaume ajitia kitanzi baada ya kuteketeza nyumba yake eneo la Gichugu

Tom Mathinji

Viongozi wa kaunti ya Murang’a wampendekeza Peter Kenneth kwa wadhifa wa naibu rais

Tom Mathinji

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi