Gavana wa Wajir Mohamed Abdi Mohamud abanduliwa

Bunge la Senate limepiga kura kuunga mkono kubanduliwa wadhifani kwa Gavana wa Wajir Mohamed Abdi Mohamud.

Licha ya kuwa Mohamud alikanusha madai yaliyolimbikiziwa dhidi yake na bunge la kaunti ya Wajir, Maseneta walipiga kura Jumatatu usiku  kumuondoa mamlakani Gavana huyo.

“Matokea ya upigaji kura nikama yafuatavyo, waliosusia ni 4, waliopinga ni 2 na waliounga mkono ni 25. Bunge la Senate limeazimia kumuondoa mamlakani Mohamed Abdi Mohamud kuwa Gavana wa kaunti ya Wajir. Gavana huyo sasa haruhusiwi kushikilia wadhifa huo,” alitangaza Spika wa bunge la Senate  Ken Lusaka baada ya zoezi la upigaji kura.

Also Read
Kiwango cha maambukizi ya Korona chafikia asilimia 5.9 humu nchini
Also Read
Wazazi wa watoto wenye ulemavu wahimizwa kutowabagua

Maseneta waliunga mkono hatua ya bunge la kaunti ya Wajir ya kumfurusha Gavana huyo baada ya kuwa na msingi dhabiti dhidi ya madai yaliyomghubika.

Miongoni mwa madai dhidi ya Mohamud ni ukiukaji wa katiba.

Kamati iliyoongozwa na Seneta wa Nyamira Okon’go Omogeni, ilipendekeza kubanduliwa kwa Mohamud baada ya kuridhika kuwa alikiuka sheria kuhusu serikali za kaunti, sheria kuhusu ununuzi na sheria kuhusu usimamizi wa pesa za umma.

Also Read
Wafugaji wanne wauliwa Turkana huku mifugo 350 wakiibwa

Mohamud amekuwa Gavana wa tatu kubanduliwa hapa nchini baada ya Mike Sonko wa Nairobi na Ferdinand Waititu wa Kiambu kutimuliwa.

  

Latest posts

Wanjigi: Kenya haina uwezo kuwapa wasio na ajira shilingi 6,000 kila mwezi

Tom Mathinji

Mwanaume ajitia kitanzi baada ya kuteketeza nyumba yake eneo la Gichugu

Tom Mathinji

Viongozi wa kaunti ya Murang’a wampendekeza Peter Kenneth kwa wadhifa wa naibu rais

Tom Mathinji

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi