Geita Gold Fc Yakosa Mihela

Timu ya soka ya Geita Gold Fc imekosa pesa nyingi ambazo ilikuwa imeahidiwa na Bi. Zahra Michuzi ambaye ni mkurugenzi wa halmashauri ya mji wa Geita na Boss wa Geita Gold FC ambayo inamilikiwa na Halmashauri hiyo. Ahadi hiyo ilitolewa muda mfupi kabla ya mechi ya leo kati ya Geita Gold SC na Simba Sc ambapo alichapisha bango la majina ya wachezaji na kuandika “Pochi ya mama imefunguka
na ushindi wa leo dhidi ya Simba SC natangaza kuununua kwa million 30 za Tanzania.”

Also Read
Samata atua Uturuki kwa matao ya Juu na kucheka na nyavu mara mbili
Also Read
Rais Samia Hassan Asuluhisha soka ya wanawake kwa kutoa ufadhili wa shilingi milioni 10 kwa mashindano ya CECAFA

Mechi hiyo iliyogaragazwa uwanjani Kirumba huko Mwanza ilikamilika sare ya bao moja kwa moja na kupitia akaunti yao ya Instagram, Geita Gold imesema imejizatiti lakini ndivyo sivyo. Wameelezea kwamba lengo lao lilikuwa kuondoka na alama tatu muhimu lakini haikuwezekana. Wamesema sasa wanarejea kujiandaa kwa mechi zijazo.

Also Read
Baraza la Sanaa la Taifa - BASATA Latoa Orodha ya Vipengele Vya Tuzo za Muziki

Bao la Geita Gold lilijiri dakika ya 20 na lilipigwa na mchezaji George “Amani” Mpole

  

Latest posts

Mchezaji Sopu Ajiunga na Azam FC

Marion Bosire

Uganda yakanusha kupiga jeki Kundi la TPLF

Tom Mathinji

Morans yang’olewa kwa mechi za kufuzu kwa kombe la dunia

Tom Mathinji

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi