George Koimburi ndiye mbunge mpya wa Juja

Mwaniaji wa Chama cha People’s Empowerment Party (PEP) George Koimburi, ameibuka mshindi katika kinyang’anyiro cha kiti cha eneo bunge la Juja.

kulingana na matokeo yaliyotangazwa na tume huru ya uchaguzi na mipaka Koimburi alijipatia kura 12,159 dhidi ya mshindani wake wa karibu Susan Njeri Waititu wa chama cha Jubilee ambaye alijipatia kura 5,746.

Joseph Gichui,aliyekuwa  mwaniaji huru alijipatia kura 1,356 kwenye uchaguzi huo mdogo uliokumbwa na idadi ndogo ya wapiga kura ya asilimia 18.9 ya jumla ya wapiga kura 115,632 waliosajiliwa katika eneo bunge hilo huku wapiga kura 21,862 pekee wakijitokeza kumchagua kiongozi wao mpya.

Uchaguzi huo mdogo uliovatutia wawaniaji 11 ulikumbwa na madai ya kuwahonga wapiga kura  na wizi wa kura, madai ambayo tume ya IEBC ilikanusha.

Mapema Jumatano asubuhi, Susan Waititu wa chama cha Jubilee aliwaongoza wafuasi wake kuondoka kwenye shughuli ya kuhesabu kura akisema uamuzi tayari ulikuwa umeafikiwa kumpendelea mpinzani wake mkuu.

Walitaka kura hizo zihesabiwe upya wakisema kura kutoka vituo vinne vya kupigia kura hazijulikani ziliko.

Akiongea Jumatano asubuhi katika kituo cha kujumuisha kura cha Mangu, mwenyekiti wa IEBC wafula chebukati alisema polisi wameanza kuchunguza kisa cha Jumanne usiku ambapo Gavana wa kaunti ya Kiambu James Nyoro aliwaongoza wahuni katika kuvurugha shughuli ya kuhesabu kura.

Kiti cha eneo bunge la Juja kilisalia wazi kufuatia kifo cha Francis Waititu kilichotokana na saratani ya ubongo mwezi Februari mwaka huu.

  

Latest posts

Mutahi Kagwe: Wahudumu wa afya wafeli katika somo la Kingereza

Tom Mathinji

Prof Magoha: Awamu ya kwanza ya ujenzi wa madarasa ya CBC kukamilika mwezi Aprili mwakani

Tom Mathinji

Benki ya dunia kuipa Kenya shilingi bilioni 16.7 kukabilia na ukame

Tom Mathinji

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi