Ghana Black Satelites wafuzu fainali ya AfFCON U 20 wakiwinda kombe la 4

Timu ya Ghana Black Satelites ilifuzu kwa fainali ya makala ya 16 ya kombe la Afrika kwa chipukizi wasiozidi umri wa miaka 20 nchini Mauritania baada ya kulipiza kisasi na kuwalemea Gambia Gambia bao 1 kwa bila lililofungwa kipindi cha kwanza kupitia kwa mkwaju wa adhabu uliopachikwa na Prince Boah.

Also Read
Harambee Stars kuondoka nchini Jumamosi kwa mchuano wa marudio dhidi ya Comoros

Nusu fainali hiyo ilisakatwa mjini Nouakchott huku Gambia wakilipia vikali baada ya kuilaza Ghana mabao 2-1 katika hatua ya makundi na kuibuka ya pili huku Ghana wakiambulia nafasi ya tatu.

Also Read
Rayton Okwiri apata ufadhili kutoka kampuni ya kamari ya 22BET kufanya mazoezi Marekani

Itakuwa mara ya kwanza kwa Ghana kupiga fainali ya kombe hilo tangu mwaka 2013 waliponyukwa na Misri kupitia penati huku wakiwinda kommbe la kwanza tangu mwaka 2009 .

Also Read
Comoros yaitoa Kenya Pumzi Kasarani

Gambia itacheza mechi ya kuwania nafasi ya tatu nne.

  

Latest posts

Tusker Fc wailewesha Gor Mahia na kutwaa kombe la FKF Supa

Dismas Otuke

Sarah Achieng’ kuzichapa dhidi ya Ruth Chisale wa Malawi kuwania mkanda wa Commonwealth Oktoba 2

Dismas Otuke

Gor Mahia yasajili wachezaji 7 tayari kwa msimu mpya

Dismas Otuke

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi