Ghana waning’inia kubanduliwa mapema AFCON kufuatia sare ya 1-1 na Gabon

Mabingwa mara nne wa kombe la AFCON ,Blackstars kutoka Ghana wanakabiliwa na hatari ya kubanduliwa mapema katika hatua ya makundi ya maakal ya mwaka huu nchini Cmaeroon,  baada ya kulazimishwa kwenda sare ya goli 1-1 na Gabon katika mchuano wa kundi C uliosakatwa Ijumaa usiku ugani Stade Ahmadou Ahidjo,Yaoundé.

Also Read
Mazishi ya aliyekuwa Rais wa Ghana Jerry Rawlings kufanyika tarehe 27 Januari

Andrew Ayew alikuwa ameiweka Ghana uongozini dakika ya 18 ya mchezo kabla ya Gabon kusawazisha katika dakika ya 88 kupitia kwa Jim Allevinah na kulazimu sar,e ambayo inatosha kwa Gabon kufuzu kwa raundi ya 16 bora wakiwa na alama 4,huku Ghana wakiwa hawana budi kuishinda Comoros kwa idadi kubwa ya mabao Jumanne ijayo iliyo kufuzu kwa raundi ya pili ,baada ya kupigwa na Moroko bao 1-0 katika pambano la ufunguzi.

Also Read
Magereza na GSU wahifadhi taji za ligi kuu Voliboli

Mchezaji wa Benjamin Teteh aliyechukua nafasi ya Andrew Ayew alilishwa kadi nyekundu mwishoni mwa mechi baada ya kumpiga ngumi mchezaji wa Gabon katika mechi hiyo.

Also Read
Wizkid kushirikiana na mwanamuziki Bella Shmurda

Moroko wamefuzu kwa raundi ya 16 bora wakiongoza kundi C kwa aalama 6 ,kufuatia ushindi wa 2 -0 Ijumaa dhidi ya Moroko,wakifuatwa na Gabon kwa pointi 4 wakati Ghana ikisalia ya tatu kwa alama 1 pekee.

  

Latest posts

Riadha Kenya kuandaa seminaa kwa wanariadha Januari 21 kutangulia mashindano ya kitaifa

Dismas Otuke

Kenya haitatuma timu kwa michezo ya Olimpiki ya majira ya Baridi Beijing

Dismas Otuke

Dagorreti North Super Cup yaingia hatua ya mwondoano

Dismas Otuke

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi