Ghana watimuliwa AFCON bila kushinda mechi kufuatia kipigo cha Comoros cha 2-3

Mabingwa mara nne wa kombe la AFCON ,Ghana maarufu kama Black Stars waliyaaga mashindano ya mwaka huu nchini Cameroon bila kushinda mechi kwa mara ya kwanza,baada ya kutitigwa mabao 3-2 na Comoros katika pambano la mwisho la kundi C Jumanne usiku ugani Romde Adja Garroua .

Comoros wanaoshiriki AFCON kwa mara ya kwanza,waliandikisha historia wakijipatia bao la kwanza kunako dakika ya 4 kupitia kwa El Fardou Ben Nabouhane, naye Ahmed Mogni akaongeza la pili dakika ya 62,kabla ya Richmond Boakye kukomboa bao moja kwa Black Stars dakika mbili baade.

Also Read
Ahly kuanza kutetea kombe la ligi ya mabingwa dhidi ya El Merreikh
Comoros wakisherehekea ushindi

Alexander Djiku alisawazisha kufanya mambo kuwa 2-2 dakika  ya 77 ,lakini matumaini ya Ghana kupata ushindi yakazimwa dakika ya 88 baada ya Ahmed Mogni kupachika wavuni bao la tatu.

Also Read
Leeds Youngstars watwaa kombe la BYSA mwaka 2021 Budalang'i baada ya kuwabwaga Subi Youngstars

Ghana waliyaaga mashindano wakiwa na pointi moja pekee na matokeo hayo ndio mabovu zaidi na huenda yakatokana na makosa ya kocha Milovan Rajevac kuwajumuisha wachezaji 17,  limbukeni katika kikosi cha AFCON.

Kwenye pambano jingine la kundi C Moroko ,Atlas Lions walitoka nyuma mara mbili na kulazimisha sare ya mabaoa 2-2 na kuongoza kundi hilo kwa pointi 7.

Also Read
Nafasi ya Kenya kwenda AFCON 2022 yadidimia baada ya kukabwa koo na Comoros

Katika mechi za mapema Jumanne katika kundi B, Zimbabwe waliwagutusha Guinea kwa kuwacharaza mabao 2-1 na kusajili ushindi wa kwanza ,huku Senegal ikilazimishwa sare tasa  na  Malawi.

Mataifa yaliyofuzu kwa raundi ya 16 bora ni Cameroon na Burkina Faso kutoka kundi A,Senegal na Guinea kutoka kundi B,Morocco na Gabon kutoka kundi C,na  Nigeria kutoka kundi D,

 

 

  

Latest posts

Barkane na Pirates kukabana koo Ijumaa fainali ya kombe la shirikisho

Dismas Otuke

Kimeli na Cheptai waibuka mabingwa wa mbio za kilomita 10 za Bengaluru

Dismas Otuke

Timu ya KPA Yakosa Kuingia Fainali

Marion Bosire

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi