Ghana yatwaa kombe la 4 la AFCON U 20 kwa kuilaza Uganda 2-0

Timu ya taifa ya Ghana maarufu kama Black satelites ndio mabingwa wa makala ya 16 ya kombe la bara Afrika kwa chipukizi wasiozidi umri wa miaka 20 baada ya kucharaza Uganda Hippos magoli 2-0 kweny fainali iliyosakatwa uwanjani Olympic mjini Noukchott Mauritania Jumamosi usiku.

Also Read
FIFA yapiga marufuku mashirikisho ya soka ya Chad na Pakistan

Uganda Hippos waliokuwa wakishiriki michuano hiyo kwa ra ya kwanza walianza kwa utepetevu na kukosa maarifa  na kumruhusu nahodha Daniel Afriye kuiweka Ghana uongozini katika dakika ya 22  akiunganisha pasi yake Fattaw Issakhu na kuongoza hadi mapumzikoni.

Also Read
Uganda kuwahifadhi wakimbizi 2,000 wa Afghanistan

Waganda walijaribu kurejea mchezoni lakini kosa la mabeki dakika ya 51 likampa Afriye fursa ya kutanua uongozi wa Ghana kwa goli la pili matokeo yaliyodumu hadi kipenga cha mwisho.

Mshambulizi wa Uganda Derrick Kakooza aliibuka mfungaji bora kwa magoli 5 huku kocha Morley Byekwaso akitawazwa kocha bora wa mashindano hayo.

Also Read
Guinea waipiga kumbo Rwanda na kutinga nusu fainali CHAN

Ilikuwa mara ya kwanza kwa Ghana kunyakua kombe hilo tangu mwaka 2009 na kusawazisha rekodi ya Black Stars ambayo pia imetwaa kombe la Afrika mara 4.

 

  

Latest posts

Tusker Fc wailewesha Gor Mahia na kutwaa kombe la FKF Supa

Dismas Otuke

Sarah Achieng’ kuzichapa dhidi ya Ruth Chisale wa Malawi kuwania mkanda wa Commonwealth Oktoba 2

Dismas Otuke

Gor Mahia yasajili wachezaji 7 tayari kwa msimu mpya

Dismas Otuke

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi