Ghasia zaendea kushuhudiwa Uswidi katika mji wa Norrköping

Ghasia zimeshuhudiwa kwa siku ya nne mfululizo kwenye miji kadhaa nchini Sweden, kufuatia kisa cha kuteketeza Kuran tukufu na kundi moja la watu wenye saisa kali za kupinga wahamiaji.

Taarifa za vyombo vya habari nchini humo zinasema watu watatu walijeruhiwa Jumapili kwenye mji wa Mashariki wa Norrköping  baada ya polisi kufyatua risasi hewani katika juhudi za kuwaogofya waandamanaji.

Also Read
Juhudi za kupatanisha Serikali na makundi ya wapinagaji nchini Ethiopia zashika kasi

Magari kadhaa yaliteketezwa kwa moto huku watu wapatao 17 wakitiwa mbaroni. Siku ya Jumamosi, magari kadhaa likiwemo Bus moja yaliteketezwa kwenye mji wa kusini wa  Malmo, wakati wa mkutano wa watu wenye siasa kali za mrengo wa kulia.

Also Read
China Katika Miaka 10 iliyopita (2)

Awali serikali za Iran na Iraq ziliwaita maafisa wa kibalozi wa Sweden  kulalamikia kisa cha kuchomwa kwa Kuran tukufu.

Raia mmoja wa Sweden mwenye asili ya Denmark Rasmus Paludan, ambaye anayeongoza vugu vugu la Stram Kurs, au Nadharia kali, amedai kuhusika na uchomaji wa Kuran Tukufu na kwamba haoni haya ya kurudia kitendo hicho.

Also Read
Rais Donald Trump: Mfumo wa Uchaguzi Marekani umekumbwa na Udanganyifu

Yamkini maafisa 16 wa polisi walijeruhiwa, na magari kadhaa kuharibiwa kwenye ghasia za Alhamisi, Ijumaa na Jumamosi katika maeneo ambako kundi hilo la watu wenye misimamo mikali lilipanga mikutano, vikiwemo vitongoji vya mji mkuu Stockholm na pia katika miji ya Linköping na Norrköping.

  

Latest posts

Kiongozi wa kijeshi nchini Burkina Faso Henri Damiba atimuliwa

Tom Mathinji

Mkuu wa Junta Burkina Faso atoa wito wa utulivu nchini humo

Tom Mathinji

Maadhimisho ya miaka 73 tangu kuanzishwa kwa Jamhuri ya Watu wa China

Tom Mathinji

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi