Gigy Kafunguliwa!

Mwanamuziki na muigizaji wa Tanzania Gigy Money amefichua kwamba adhabu aliyopatiwa na baraza la sanaa la Tanzania imekamilika na sasa yuko huru kurejelea shughuli zake katika sanaa.

Adhabu hiyo ilitokana na hatua yake ya kukiuka maadili kwa namna alivyokuwa amevaa akitumbuiza jukwaani kwenye tamasha la Wasafi Festival mwanzo wa mwaka huu wa 2021.

Tukio hilo lilikuwa likipeperushwa moja kwa moja kwenye runinga ya Wasafi na kwa sababu hiyo nayo ilifungiwa kwa miezi sita na mamlaka ya mawasiliano nchini Tanzania TCRA.

Also Read
Rais wa Tanzania John Magufuli amefariki

Hata hivyo runinga ya Wasafi ilifunguliwa mwanzo wa mwezi wa tatu baada ya maombi kadhaa kwa mamlaka ya mawasiliano kutoka kwa wasimamizi wake akiwemo Diamond Platnumz.

Siku hiyo Gigy Money aliingia jukwaani vizuri akiwa amevaa dera na baadaye akalivua akabakia na vazi la kunata mwilini ambalo rangi yake ilikuwa sawa na rangi ya ngozi yake ungedhania yuko uchi.

Also Read
Harmonize kushirikiana na msanii Anjella

Gigy alitangaza kukamilika kwa adhabu yake na kupatiwa kibali na BASATA tena kwenye sherehe ya mtoto wa muigizaji wa filamu za Bongo Irene Uwoya.

Alisema atarejelea kazi kama mwanamuziki kwa mipango ambayo ataitangaza hii leo kwenye sherehe ya siku yake ya kuzaliwa.

Also Read
Wema Sepetu kuigiza kwenye filamu ya kimataifa

Kulingana na mabango ya aliowaalika kwenye tukio hilo aliyoyachapisha kwenye Instagram, sherehe itaandaliwa katika eneo la Mbezi Beach Jijini Dar es Salaam nchini Tanzania.

Diamond Platnumz, Wema Sepetu, mbwa wa Wema Manunu, Irene Uwoya, Zuchu, Mbosso na Rayvanny ni Kati ya watu ambao Gigy amewaalika kwenye sherehe ya siku yake ya kuzaliwa.

  

Latest posts

Wasanii Wanaowakilisha Kenya AFRIMA

Marion Bosire

Akothee Apata Mgeni wa Heshima Kwenye Hafla Yake

Marion Bosire

KFCB Yazuia Usambazaji Wa Filamu

Marion Bosire

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi