Gladys Erude ameaga dunia

Mtangazaji mkongwe Gladys Adisa Erude ameaga dunia. Habari za kifo chake zilitolewa na mwanawe ambaye anajiita Sly Erude kwenye Facebook.

Alipachika picha ya marehemu mamake na kutoa maelezo kwamba mama Gladys aliaga dunia tarehe 4 mwezi Agosti mwaka 2021 saa nne na dakika 15 usiku saa za Marekani.

Kulingana naye Gladys Erude amekuwa akiugua ugonjwa wa saratani na ugonjwa wa moyo kwa muda.

Also Read
Buriani Beatrice Kevogo

Gladys Adisa Erude alifanya kazi kama mtangazaji katika shirika la utangazaji nchini KBC kwa muda wa miaka 25 na alianza wakati lilikuwa likijulikana kama VOK.

Taaluma yake ya kwanza ilikuwa ualimu baada ya kufuzu kutoka Chuo kikuu Cha Kenyatta. Alikuwa akifunza katika shule ya upili ya wasichana ya Tigoi na alikuwa anapenda kusikiliza redio ambayo ilimsaidia kufahamu Kiswahili.

Alijaribu bahati yake kwenye mahojiano ya kutafuta watangazaji wa VOK na akafuzu na kubadilisha taaluma.

Also Read
Bunge lapendekeza kuanzisha kituo chake cha habari

Alipohojiwa na kituo kimoja cha runinga yapata miaka minne iliyopita, Erude alisema alistaafu kutoka KBC mwaka 2001 akaingilia biashara ya kuandaa matangazo ya kibiashara kwa miaka 7 na mwaka 2008 akasafiri hadi Marekani kuishi na wanawe.

Also Read
Gladys Erude kuzikwa tarehe 14 Agosti kaunti ya Nandi

Mume wake aliaga dunia akiwa na umri wa miaka 24 tu na kumwacha na watoto wanne. Alikosa kuelewana na jamii ya marehemu mume wake kwa sababu ya tamaduni ya kurithiwa akajinunulia shamba na kujijengea katika kaunti ya Nandi.

Ameacha watoto sita wote wa kiume na wanne kati yao wanaishi na kufanya kazi Marekani.

  

Latest posts

Kenya yanakili visa 113 vipya vya COVID-19

Tom Mathinji

Wazazi wasema watatetea mtaala mpya wa Elimu wa CBC

Tom Mathinji

Watu watano wana kesi ya kujibu dhidi ya mauaji ya wakili Willie Kimani

Tom Mathinji

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi