Gor kuanza kutetea ubingwa dhidi ya wagema mvinyo Tusker Fc

Mabingwa mara 18 wa  ligi kuu ya Kenya Gor Mahia wataanza harakati za kutetea taji hiyo dhidi ya wagema mvinyo Tusker Fc Novemba 21.

Kulingana na ratiba ya mechi za msimu wa mwaka 2020/2021 ya ligi kuu ya Betking  Kogalo wanaowania taji ya tano kwa mpigo wataanzia ugenini dhidi ya Tusker Fc

Also Read
Purity Chepkirui na Winnie Jemutai watinga fainali ya mita 1500

Gor watarejea nyumbani kwa mchuano wa pili dhidi ya wanajeshi Ulinzi Stars kabla ya kuizuru Mathare United ,kuwaalika Sofapaka na kuwazuru Bidco United katika mechi ya tano kwenye ratiba.

FKF PL FIXTURES

Hata Hivyo Ratiba hiyo iliyotangazwa inasubiri kuidhinishwa na  na wizara ya afya na ile ya michezo kuhusu ugonjwa wa covid 19.

Also Read
Kenya kuandaa makala ya kwanza ya CECAFA women Champions League

Kwa upande wao Afc Leoapards watafungua msimu wakiwania ubingwa kwa mara ya kwanza baada ya Subira ya miaka 22 ,Novemba 20 dhidi ya Western Stima nyumbani kabla kuwatembelea  Bidco United na kusafiri hadi Kericho kumenyana na  Zoo Fc Desemba  na kisha kuwaalika Nzoia Sugar siku tano baadae .

Also Read
AK Central Rift yalenga kuteua kikosi dhabiti cha chipukizi u 20

Bandari watafungua msimu nyumbani Mbaraki dhidi ya  Zoo, na kusafiri kwenda Kisumu dhidi ya  Westen Stima.

kulingana na wadadisi endapo ligi hiyo haitaanza kufikia mwishoni mwa mwezi ujao,huenda ikawa vigumu kwa msimu kumalizika kwa muda kuambatana na ratiba ya Caf.

 

 

 

 

 

 

 

 

 

  

Latest posts

Boro wamtimua meneja Chris Wilder kwa matokeo duni

Dismas Otuke

Malkia Strikers warejea nyumbani kinyemela baada ya kubanduliwa mashindano ya dunia

Dismas Otuke

CAF yafungua maombi ya maandalizi ya fainali za AFCON mwaka 2025

Dismas Otuke

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi