Gor Mahia tayari kuwashika mateka wanajeshi APR Jumamosi

Mabingwa watetezi wa ligi kuu ya Kenya Gor mahia, wana imani ya kufuzu kwa mchujo wa pili wa ligi ya mabingwa Afrika huku wakilenga ushindi unaohitajika dhidi wapinzani kutoka Rwanda Jumamosi .

Kocha wa muda wa Gor Mahia Pamzo Omolo ana imani kuwa wamejiandaa vyema  na wana uwezo wa kuishinda APR Jumamosi hii katika marudio ya  mechi ya mchujo ya kombe la ligi ya mabingwa Afrika Caf.

Omolo aliyasema haya mapema Ijumaa akiiongoza timu hiyo kwa mazoezi ya mwisho kabla  ya pambano la Kesho katika uwanja wa taifa wa Nyayo.

”Kwa sasa tumejiandaa vyema na kile tunahitaji ni kufunga bao  na kutowaruhusu kufunga ili kufuzu kwa mchujo wa pili na hili linawezekana”akasema Omolo

Kwa Upande wa nahodha Keneth Muguna amesema ,lengo lao ni kushinda pambano la Jumamosi na pia mechi itakayofuatia ili kufuzu kwa hatua ya makundi na hili litawekezekana  hususan baada ya  kurekebisha makosa ya mkumbo wa kwanza wiki iliyopita.

Also Read
Rais wa CAF Dkt Motsepe aongoza kikao cha kwanza na kuwateua wasaidizi wake

”Tuko sawa na tuna imani tutapata ushindi na kufuzu kwa next round ,tuliona makosa ya mechi ya mkumbo wa kwanza  huko Rwanda na inawezekana kucheza hadi hatua ya makundi” akasema Muguna

Meneja wa timu hiyo Jolawi Obondo ameahidi kusajili ushindi unaohitajika kesho huku akielezea imani yake na kikosi cha sasa .

Wakati uo huo Obondo amesema kushindwa kwao wiki jana mjini Kigali kulitokana na matayarisho duni ikiwemo kupata tiketi za usafiri wakiwa wamechelewa ,lakini wamesahau hayo na kile wanalenga sasa ni kuishinda APR na pia kuingia hatua ya makundi ya kombe hilo kwa mara ya kwanza.

“Katika mechi ya Rwanda tulikuwa na shida kadhaa ikiwa ni pamoja na kupata tiketi za ndege tukiwa tumechelewa na hatukupata muda wa kutosha kujiandaa tulipofika.Hata hivyo saa hii tuko sawa na kesho kazi ni kuishinda APR kisha tuingie mchujo wa pili na inawezekana kufuzu kwa group stage kwa mara ya kwanza kwa sababu niko na timu nzuri”akasema Obondo

Also Read
Yanga kuvaana na Simba ,Nani mtani wa Jembe ?

 

Meneja huyo amewarai mashabiki kuishabiki timu hiyo kesho kupitia runinga  ya Kbc Channel One kwani hawataruhusiwa kuingia uwanjani.

“Fans wetu hata ingawa hawataingia uwanjani tunawaomba kuisupport timu kwa kutazama KBC  Channel one  ambayo itaonyesha mchuano huo “akaongeza Obondo

Kogalo wanahitaji ushindi wa bao 1-0 dhidi ya APR Jumamosi ili kufuzu kwa mchujo wa pili baada ya kupoteza 1-2 wiki jana dhidi ya wanajeshi hao kwenye mkumbo wa kwanza huko Kigali.

Wakati huo huo timu hiyo imepigwa jeki baada ya kupokea jozi 40 za sare  za kufanyia mazoezi maarufu kama track suits kutoka kwa mwanasia Eliud Owalo aliyehudhuria mazoezi ya timu hiyo mapema Ijumaa.

Also Read
Burkinafasso wacheza CHAN kwa mara ya 3

 

Mwanasiasa Eliud Owalo akitoa sare za mazoezi kwa meneja wa  Gor Mahia  Jolawi Obondo  katika uwanja wa Nyayo

Owalo aliahidi kuendelea  kuiunga mkono timu hiyo na kutoa changamoto kwa wachezaji hao kujituma katika mechi ya Jumamosi na kusajili ushindi unaohitajika ili kufuzu kwa raundi nyingine huku  akielezea masikitiko yake baada ya wachezaji hao kukosa sare mazoezi katika mechi ya wiki jana na kulazimika kuvalia sare za shirikisho  hatua iliyozua utata.

“Leo nimekuja kusimama na timu na nimetoa  jozi  40 za sare za mazoezi kama njia moja ya kuwapa morali kwa mechi ya kesho.Kilichotokea wiki jana ni aibu ambapo wachezaji walikosa sare za mazoezi wakiwa Rwanda na kulazimika kuvalia sare za shirikisho.Mimi nitaendelea kutoa msaada wa hali na mali kwa timu hii “Akasema Owalo

Mshindi wa mechi  hiyo kwa jumla atafuzu kupiga na aidha mabingwa wa Algeria Cr Belouizdad au miamba wa Libya Al Nsr katika mchujo wa pili.

  

Latest posts

Dismas Otuke

Omanyala ajiunga na National Police Service

Dismas Otuke

Rais wa zamani wa shirikisho la riadha ulimwenguni IAAF Lamine Diack afariki akiwa na umri wa miaka 88

Dismas Otuke

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi