Gor Mahia watemwa nje ya kombe la shirikisho baada ya kulazimishwa sare ya 1-1 na AS Otoho D Oyo

Ndoto ya Gor Mahia kufuzu hatua ya makundi ya kombe la shirikisho ,ilizimwa Jumapili jioni, baada ya kulazimishwa kwenda sare ya bao 1-1 na wageni Otoho D Oyo ya kutoka Congo Brazaville ,katika mchuano uliosakatwa katika uga wa kitaifa wa Nyayo,na kubanduliwa kwa ushinde wa 1-2 kufuatia ushindi wa Otoho 1-0 katika duru ya kwanza.

Also Read
Kocha wa Gor Mahia Andreas Spier afunganya virago

Gor walijikuta kwenye nji panda baada ya kufungwa bao la kwanza na wageni ,kabla ya kusawazisha na kipindi cha kwanza kumalizikia sare ya 1-1 ,na timu zote kujihami kipindi cha pili chote.

Also Read
Kesi dhidi ya wakili Paul Gicheru yaanza katika Mahakama ya ICC

Kogalo walikuwa na fursa ya kufuzu kwa hatua ya makundi hususan baada ya kucheza mbele ya mashabiki waliokuwa wanarejea uwanjani kwa mara ya kwanza tangu mwaka 2019.

Otoho ambao ni mabingwa wa ligi kuu ya Congo Brazaville wamejikatia tiketi kwa hatua ya makundi ambayo kwa desturi huwa na donge nono ambapo pia gharama zote za usafiri na maandalizi ya mechi hugharamiwa na shirikisho la soka CAF.

  

Latest posts

Takwimu za kipute cha 22 cha kombe la dunia nchini Qatar

Dismas Otuke

NPS: Oparesheni ya kiusalama Turkana yazaa matunda

Tom Mathinji

Bodi ya dawa na sumu yapiga marufuku uuzaji wa dawa ya kupanga uzazi ya ‘Sophia’

Tom Mathinji

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi