Gor Mahia yasajili nembo zake 4 kwa miaka 10 ijayo

Klabu ya Gor Mahia imesajili nembo zake nne kwa kipindi cha 10 ijayo kama njia moja ya kulinda mali yake na kuzuia matumizi ya nembo hizo bila idhini.

Akizungumza wakati wa hafla ya kuzindua nembo hizo ,mweka hazina wa Gor Dolphina  Odhiambo amesema kuwa iliwachukua muda mrefu kabla ya nembo hizo kusajiliwa rasmi katika afisi ya msajili wa vyama na kuwatahadhari wale wanaotumia nembo hizo kiholela kwamba hawana budi kupata kibali kutoka kwa afisi yake.

Also Read
Gor Mahia wafanya mazoezi ya mwisho nchini Misri kabla ya mtihani wa Al Ahly Merowe ya Sudan Ijumaa

“Imechukua muda mrefu lakini hatimaye tumesajili nembo hizi nne ambapo yeyote atakayetaka kuuza jezi na sare za timu au kufanya biashara kwa kutumia nembo hizi ni sharti alipie kupitia kwa ofisi yangu”akasema Bi Odhiambo

Also Read
Gor mahia wakamatwa na wanajeshi wa Rwanda APR

Kwa upande wake mwenyekiti Ambrose Rachier amesema  ni hatua ambayo timu hiyo imepiga tangu kubuniwa mwaka 1968 na ni mwamko mpya.

“Hii ina maana kuwa wale ambao wamekuwa wakitumia nembo hizi hadi mwaka 2020  hawana tatatizo lakini wale ambao wataitumia sasa  hadi mwaka 2030 ni lazima wapitie ofisini”akasema Rachier.

Also Read
Raila ahimiza mashirika kusaidia vilabu vya kijamii

Nembo zilizosajiliwa   ni The Green Army,K’ogalo,Sirkal na Gor Mahia FC na  zilianza kutumika  Oktoba 14 mwaka 2020 hadi Oktoba 14 mwaka 2030.

  

Latest posts

Sharon Chepchumba atua Ugiriki kupiga Voliboli ya kulipwa kwa miezi sita

Dismas Otuke

Boro wamtimua meneja Chris Wilder kwa matokeo duni

Dismas Otuke

Malkia Strikers warejea nyumbani kinyemela baada ya kubanduliwa mashindano ya dunia

Dismas Otuke

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi