Gor Mahia yasajili wachezaji 7 tayari kwa msimu mpya

Klabu ya Gor Mahia imewazindua wachezaji 7 wapya inapojiandaa kwa msimu wa ligi kuu nchini FKF mwishoni mwa juma hili.

Wing’a Boniface Omondi
Mshambulizi Peter Lwasa

Wanandinga hao wapya wanawajumuisha watano kutoka humu nchini na wawili wa kigeni huku sita kati yao wakisaini kandarasi za miaka miwili kila mmoja .

Also Read
Vipusa wa Kenya tayari kutetemesha ardhi mashindano ya dunia ya nusu marathon Jumamosi hii
Kipa Adama Keita kutoka Guinea

Kogalo imemsajili mlinda lango Adama Keita kutoka klabu ya Indastriel de Kamsar ya Guinea kwa mkataba wa miaka miwili na mshmabulizi Sando Yangayay anayetokea timu ya Aguila ya DRC kwa mkataba wa miaka miwili pia .

Also Read
Christian Ericksen Azirai uwanjani na kulazimu mechi ya Euro kati ya Denmark na Finland kusimamishwa
Mshambulizi  Sando Yangayay kutoka DRC
Beki Dennis Nganga

Wachezaji wengine waliotua katika ngome ya the Green army ni mabeki Dennis Nganga kutoka Wazito Fc,Joshua Onyango kutoka Kariobangi Sharks,kiungo Peter Oudu wa Kariobango Sharks,mshmabulizi Peter Lwasa pia kutoka Kariobangi Sharks na Wing’a Boniface Omondi wa WazitO Fc.

  

Latest posts

Boro wamtimua meneja Chris Wilder kwa matokeo duni

Dismas Otuke

Malkia Strikers warejea nyumbani kinyemela baada ya kubanduliwa mashindano ya dunia

Dismas Otuke

CAF yafungua maombi ya maandalizi ya fainali za AFCON mwaka 2025

Dismas Otuke

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi