Gor wazidi kutota ligini baada ya kushindwa na Posta Rangers

Mabingwa watetezi wa ligi kuu ya Kenya Gor Mahia waliendeleza msururu wa matokeo duni ligini baada ya kuambulia kichapo cha pili mtawalia walipolazwa na Posta Rangers bao 1-0 katika mojawapo wa mchuano wa ligi uliosakatwa katika uwanja wa Kasarani Jumatano alasiri.

Also Read
Sharks yaweka hai matumaini ya kuwania taji ya ligi kuu baada ya kuinyofoa Mathare United 2-1

Kiungo Francis Nambute alipachika bao la pekee la ushindi kwa Rangers dakika ya kwanza ya ziada katika kipindi cha kwanza, huku Kogalo wakipoteza nafasi  nyingi za kusawazisha  hadi kipenga cha mwisho.

Ilikuwa mechi ya pili mtawalia kwa Gor kupoteza na ya sita msimu huu baada ya ksuhindwa na  KCB mabao 2-0 mwishoni mwa juma lililopita.

Also Read
KBC Channel 1 kupeperusha mechi ya Kenya dhidi ya Zambia Ijumaa

Gor Mahia ingali ya 8 ligini kwa pointi 19  na watarejea uwanjano Machi 21 dhidi ya Bidco United.

Also Read
Michezo yafungwa kote nchini

Rangers kwa upande wao wamepanda hadi nafasi ya 14 kwa alama 14 kufuatia ushindi huo.

Katika pambano jingine la Jumatano Zoo Fc ya Kericho na Western Stima walitoka sare tasa katika uwanja wa Kericho Green.

  

Latest posts

Police Fc washerehekea kurejea ligi kuu baada ya mwongo mmoja kwa dhifa

Dismas Otuke

Sportpesa kurejesha ufadhili michezo nchini Kenya

Dismas Otuke

Vidosho wa Kenya wapigwa dafrao na Msumbiji mashindano ya kikapu Afrika

Dismas Otuke

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi