GOR,AFC waitaka serikali kutotekeleza ushuru wa asilimia 20 kwa kampuni za kamari

Ushuru huo wa asilimia 20 ulikataliwa  mwaka 2019, baada ya bunge kuangusha mswaada huo wa fedha ,kabla ya waziri wa fedha Ukur Yattani kutangaza kurejeshwa kwa ushuru huo wiki jana alipokuwa akisoma bajeti.

Wenyeviti wa Gor Mahia na AFC leopards wameiomba serikali kubadili uamuzi  wa kutekeleza ushuru wa mpya wa asilimia 20 kwa kampuni zote za mchezo wa kamari nchini ,wakiongeza kuwa  ushuru huo utaziumiza timu  zinazotegemea ufadhili wa kampuni kama hizo .

Mwenyekiti wa Leopards Dkt Dan Shikanda  amesema kuwa taifa lingali linapambana na hali ngumu iliyoletwa na janga la covid 19 na  si  busara kwa serikali kutekeleza ushuru huo mpya.

“Kile tunachoomba kwa sasa ni serikali isitekeleze ushuru huu mpya kwani utaathiri wafadhili wetu ,na mzigo huo wataurudisha kwetu tunaowategemea “akasema Dkt Shikanda

Also Read
Watu 2,964 zaidi wabainishwa kuwa na Covid-19 hapa nchini

Upande wake Ambrose Rachier ambaye ni mwenyekiti wa Gor Mahia amesema uamuzi huo huenda ukawalazimu wafadhili wao kampuni ya BETSAFE kusitisha  au kupunguza ufadhili wao kwa  timu hizo hali ambayo itaongeza mzigo kwa vilabu hivyo.

“Kwetu Gor Mahia,na Afc Leopards na timu nyingine chache wafadhili tayari wametekeleza majukumu yao ya kutufadhili na kutimiza malengo  yao msimu huu,na tunaitaka serikali  na wabunge kutotekeleza ushuru huo mpya ambao utawafurusha wafadhili”

Also Read
Mtihani wa KCPE wavurugwa kaunti ya Baringo

Wenyeviti hao ambao pia timu zao zitachuana katika fainali ya kombe la fkf tarehe 4 mwezi ujao ,wameomba serikali kuruhusu fainali hiyo kuandaliwa katika uwanja wa taifa wa nyayo na pia mechi nyingine za ligi kuu ,badala ya viwanja vinavyotumiwa kwa sasa ambavyo vinahatarisha maisha  ya wachezaji kutokana na hali  yao mbovu .

“Nichukue fursa hii kuirai serikali kuruhusu tutumie uwanja wa nyayo kwa fainali ya fkf cup au Betsafe Derby,soka itachezwa vipi bila uwanja bora,tunaomba serikali na vyombo vya habari kuhakikisha fainali hii ya Julai 4 na mechi nyingine za soka zinachezewa uwanja wa Nyayo na pia kasarani ambayo ni vya hadhi ya kimataifa”akaongeza Shikanda

Also Read
Harambee Stars yazabwa kofi na Mali nchini Moroko na kuandikisha kipigo cha kihistoria

Ushuru huo wa asilimia 20 ulikataliwa  mwaka 2019, baada ya bunge kuangusha mswaada huo wa fedha ,kabla ya waziri wa fedha Ukur Yattani kutangaza kurejeshwa kwa ushuru huo wiki jana alipokuwa akisoma bajeti.

  

Latest posts

Malkia Strikers wabanduliwa mashindano ya dunia baada ya kipigo cha seti 3-1 na Puerto Rico

Dismas Otuke

Boubacar Kamara kutocheza kwa muda kutokana na Jeraha

Tom Mathinji

Familia ya Mbijiwe yatoa wito kwa Rais Ruto kusaidia kumpata mwana wao

Tom Mathinji

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi