Gucci Mane asajili mwanamuziki mwingine

Mwanamuziki wa mtindo wa rap nchini Marekani Radric Delantic Davis maarufu kama Gucci Mane ni mmoja wa wanamuziki maarufu sana kwenye ulingo wa muziki wa Hip-Hop na anaendesha pia kampuni ya kurekodi muziki na kusimamia wanamuziki.

Kwa sasa anaonekana kuanza kuvizia talanta kati ya vijana wa umri mdogo kupitia kwa kampuni yake ya muziki iitwayo “1017 Global Music LLC”.

Also Read
Nick Cannon Asema Anatarajia Watoto Zaidi Mwaka Huu

Kufikia sasa amesajili wanamuziki kama Pooh Shiesty, Foogiano na Big Scarr kati ya wengine. Aliyemwongeza hivi karibuni kwenye orodha ya wasanii anaosimamia ni mwanafunzi wa shule ya upili wa umri wa miaka 18 ambaye anaitwa “Bic Fizzle”. Gucci Mane alitangaza hayo kupitia Instagram.

Also Read
Ndoa ni utumwa! Chris Kirubi

mane alipachika video fupi kwenye akaunti yake ya Instagram ambayo inaonyesha akimkabidhi Bic Fizzle mkufu na kuandika ‚ÄúNimemsajili jamaa mdogo toka Arkansas. Ana umri wa miaka 18 tu na yuko katika gredi ya 12 na anacheza mpira kwenye timu ya shule.”

Mashabiki wa Gucci Mane sasa wanasubiria muziki mzuri kutoka kwa Bic Fizzle chini ya usimamizi wa Gucci. Mane wa umri wa miaka 41 sasa alianzisha kampuni ya 1017 Global Music, LLC mwaka 2007, baada ya kuondoka kwenye kampuni iliyokuwa ikimsimamia ya Mizay Entertainment na baada ya kufungwa kwa nyingine iliyokuwa ikiitwa “So Icey”.

  

Latest posts

Harusi ya Nandy Kuwa ya Awamu Tatu

Marion Bosire

Mwigizaji Mkongwe wa Nollywood Kenneth Aguba Apata Usaidizi

Marion Bosire

Travis Baker Arejea Kazini

Marion Bosire

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi