Guinea yaondolewa katika Jumuiya ya ECOWAS

Jumuiya kuu ya Kiuchumi ya Mataifa ya Afrika Magharibi (ECOWAS) imesimamisha uanachama wa taifa la Guinea, siku chache baada ya mapinduzi ya kijeshi ambayo yalimuondoa mamlakani Rais Alpha Conde wa nchi hiyo.

Kwenye mkutano usio wa kawaida wa viongozi wa mataifa wanachama wa Jumuiya hiyo ulioandaliwa kwa njia ya mtandao, viongozi hao walitaka kurejelewa kwa utaratibu wa kikatiba nchini Guinea na kuachiliwa mara moja kwa Conde, ambaye alikamatwa na Kikosi Maalum kilichoongozwa na Luteni Kanali Mamady Doumbouya mnamo Jumapili.

Also Read
Ufaransa yafunga shule kwa wiki tatu kudhibiti msambao wa Covid-19
Also Read
Tanzania yagura CHAN baada ya kuwahemesha Guinea

Viongozi wa mataifa wanachama wa jumuiya ya ECOWAS pia walikubali kutuma ujumbe wa ngazi ya juu nchini Guinea leo kabla ya jumuiya hiyo kuchunguza tena msimamo wake.

Also Read
Wananchi wa Guinea wapiga kura kumchagua rais

Uamuzi huo umetokea baada ya mapinduzi hayo kuzua shutuma kubwa za kidiplomasia, huku pia yakishangiliwa katika baadhi ya sehemu za mji mkuu wa taifa hilo, Conakry, ambapo wakazi walijitokeza barabarani kushangilia wanajeshi.

  

Latest posts

Idadi ndogo ya wakazi wa Nairobi wajitokeza kuchanjwa dhidi ya COVID-19

Tom Mathinji

Watumishi wa Umma wahimizwa kushirikisha taasisi mbali mbali kufanikisha majukumu yao

Tom Mathinji

Aliyekuwa Rais wa Algeria Abdelaziz Bouteflika amefariki

Tom Mathinji

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi