Guinea yaondolewa katika uanachama wa Muungano wa Afrika

Muungano wa Afrika umeondoa Guinea kwenye uanachama wa muungano huo kufuatia mapinduzi yaliyotekelezwa Jumapili. Hayo yamesemwa kwenye mtandao wa Tweeter wa idara ya amani na usalama ya muungano huo.

Rais  Alpha Condé aliondolewa mamlakani na kundi la wanajeshi linaloongozwa na kanali  Mamady Doumbouya. Mapinduzi hayo yameshtumiwa na viongozi wa kanda hiyo,  muungano wa Afrika , katibu mkuu wa umoja wa mataifa na  Marekani.

Also Read
Bush ampongeza Biden kwa ushindi wa kura za Urais Marekani
Also Read
Utawala wa kijeshi Myanmar kudumu hadi Agosti 2023

Shirika la ECOWAS lilitangulia kuiondoa nchi hiyo kwenye uanachama wake siku ya Jumatano huku mawaziri wa mataifa ya kanda ya Afrika Magharibi wakiwasili Jijini  Conakry kujadili hali ya kurejesha mfumo wa kikatiba.

Also Read
Tanzania yagura CHAN baada ya kuwahemesha Guinea

Taarifa hiyo pia ilimtaka Rais wa tume ya Umoja wa Afrika Moussa Faki, kushauriana na wadau katika kanda hiyo kwa lengo la kutatua zogo hilo linaloghubika taifa la Guinea.

  

Latest posts

Aliyekuwa Rais wa Algeria Abdelaziz Bouteflika amefariki

Tom Mathinji

Ethiopia yakaribisha wito wa kurejelewa mazungumzo na majirani wake kuhusu bwawa katika mto Nile

Tom Mathinji

Bwawa katika mto Nile lazidisha uhasama kati ya Ethiopia, Sudan na Misri

Tom Mathinji

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi