Guterres aahidi kuangazia mabadiliko ya hali ya anga ulimwenguni

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres ameapa kulipa kipaumbele suala la mabadiliko ya hali ya anga katika Umoja huo.

Guterres amesema wanadamu wanaedeleza uharibifu wa mazingira na kusababisha madhara makubwa.

Also Read
Wapiganaji wa kigeni watakiwa kuondoka nchini Libya

Katika hotuba yake wakati wa kikao maalum kuhusu mazingira, Guteres amesema lengo lake kuu mwaka ujao ni kutafuta muungano wa mataifa duniani ili kushinikiza kwa pamoja juhudi za kukomesha kabisa uchafuzi wa mazingira duniani.

Also Read
Umoja wa Mataifa wakashifu mauaji ya raia nchini Myanmar

Hatua hii itawezesha kupunguzwa kwa kiwango cha gesi zinazochafua hewa na pia kuhakikisha usafi wa gesi ambayo huenda ikafuka hewani.

Guterres amesema kila taifa, jiji, mashirika ya kifedha na kampuni ni sharti ziweke mipango ya kupunguza kiwango cha gesi inayofuka hewani kufikia mwaka wa 2050.

Also Read
Afisi ya mkurugenzi wa mashtaka ya umma yapongezwa kwa kukumbatia mfumo wa dijitali

Amesema kuwa wadau hao watahitajika kuweka mikakati ifaayo ili kufanikisha maono hayo.

  

Latest posts

Mgomo wa wahudumu wa afya wasababisha maafa Guinea Bissau

Tom Mathinji

Aliyekuwa Rais wa Algeria Abdelaziz Bouteflika azikwa Jijini Algiers

Tom Mathinji

Aliyekuwa Rais wa Algeria Abdelaziz Bouteflika amefariki

Tom Mathinji

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi