Haji aidhinisha kushtakiwa kwa wahusika wa sakata ya zabuni za usambazaji umeme

Mkurugenzi Mkuu wa Mashtaka ya Umma Noordin Haji ameidhibisha kushtakiwa kwa watu wanane na kampuni mbili kuhusiana na ufujaji wa zaidi ya shilingi milioni 103.

Fedha hizo zilikuwa zimenuiwa kutekeleza mradi wa kuweka umeme wa sola na, chini ya Kampuni ya Usambazaji Umeme Mashinani.

Wanane hao ni pamoja na aliyekuwa Afisa Mkuu Mtendaji wa kampuni hiyo Nofatos Munyu, James Muriithi (Mkuu wa Kawi), Joel Omusembe (Mkuu wa Kitengo cha Utoaji Zabuni), Simon Kirui (Mchumi), Mkurugenzi wa Kampuni ya Nav World Limited Abdirahman Dakane na Wakurugenzi wawili wa Kampuni ya North Pride Limited Hassan Sheikh Mohammed na Fatuma Abdi Hassan.

Also Read
Je, ni nani atashtakiwa katika kashfa ya Mabwawa ya Arror na Kimwarer?

Nazo kampuni mbili zinazochunguzwa kuhusiana na sakata hiyo ni North Pride Limited na Nav World Limited.

Mashtaka yanayowakabili ni pamoja na kupanga njama ya kutekeleza uhalifu wa ufisadi, matumizi mabaya ya mamlaka, kutozingatia sheria za utoaji zabuni kwa kukusudia na kujipatia mali za umma kimagendo.

Kwenye taarifa, Tume ya Maadili na Kupambana na Ufisadi (EACC) imethibitisha kukamatwa kwa Nofatos Munyu, James Muriithi, Joel Omusembe na Simon Kirui mapema leo.

Also Read
Tume ya EACC yakana madai ya kuvamia afisi ya Wakili John Khaminwa

Tume hiyo kwa sasa bado inawasaka washukiwa waliosalia na imewashauri kujisalimisha ili kufanyiwa uchunguzi.

Kulingana na wapelelezi wa EACC, kampuni za Nav World Limited na North Pride Limited hazikutuma maombi ya kuidhinishwa na kuorodheshwa miongoni mwa kampuni zinazoweza kupewa zabuni ya kusambaza umeme wa solar kwa shule za umma nchini.

Licha ya hivyo, aliyekuwa Afisa Mkuu Mtendaji wa Kampuni ya Usambazaji Umeme Mashinani Nofatos Munyu anadaiwa kuidhinisha kampuni hizo na baadaye kuzipatia kandarasi za kutekeleza mradi huo kwa gharama ya shilingi 39,896,018 na 46,957,685 mtawalia.

Also Read
Maafisa wa Wizara ya Kilimo wakabiliwa na mashtaka ya ufisadi

Wapelelezi hao pia waligundua kwamba Kampuni ya Nav World Limited ilisajiliwa na Msajili wa Kampuni tarehe 2 mwezi Septemba mwaka wa 2014, takriban miezi mitatu baada ya makataa ya kampuni kuwasilisha stakabadhi zao kwa ajili ya zabuni hizo.

“Kufuatia kukamilika kwa uchunguzi, EACC inapendekeza kwamba maafisa wa Kampuni ya Usambazaji Umeme Mashinani pamoja na Wakurugenzi wa Kampuni za Nav World na North Pride Limited wafunguliwe mashtaka,” ikasema taarifa ya tume hiyo.

  

Latest posts

Wanjigi: Kenya haina uwezo kuwapa wasio na ajira shilingi 6,000 kila mwezi

Tom Mathinji

Mwanaume ajitia kitanzi baada ya kuteketeza nyumba yake eneo la Gichugu

Tom Mathinji

Viongozi wa kaunti ya Murang’a wampendekeza Peter Kenneth kwa wadhifa wa naibu rais

Tom Mathinji

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi